BENKI YA NBC YASHAURIWA KUONGEZA VITUO VYA HUDUMA ZA KIBENKI MKOANI PWANI

BENKI YA NBC YASHAURIWA KUONGEZA VITUO VYA HUDUMA ZA KIBENKI MKOANI PWANI

Na. Wellu Mtaki  Pwani Jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa  wa pwani yaiomba Benki ya NBC kuongeza vivutio Ili wafanyabiashara kujiunga na bank hiyo huku  wafanyabiashara wa mkoa wa pwani wakiwahakikishia bank hiyo kuwa watakuwa  na ushirikiano mkubwa kuazia sasa. Hayo yamezungumzwa na wafanyabiashara wakati wa warsha ya wafanyabiashara na bank ya NBC  mkoani pwani iliyojumuisha

Na. Wellu Mtaki  Pwani


Jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa  wa pwani yaiomba Benki ya NBC kuongeza vivutio Ili wafanyabiashara kujiunga na bank hiyo huku  wafanyabiashara wa mkoa wa pwani wakiwahakikishia bank hiyo kuwa watakuwa  na ushirikiano mkubwa kuazia sasa.


Hayo yamezungumzwa na wafanyabiashara wakati wa warsha ya wafanyabiashara na bank ya NBC  mkoani pwani iliyojumuisha wawakilishi 60 toka wilaya tofauti tofauti mkoa wa pwani. Pamoja na kuweka ushirikiano Kati ya Jumuiya ya wafanyabiashara na bank hiyo.


KWa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa pwani Abdallah Ndauka amesema ni wakati sasa wa Benki ya NBC kutumia fursa zilizopo mkoani pwani kama jinsi pwani ilivyo na taswila ya pwani ya viwanda kushirikiana na wafanyabishara kuongeza uchumi wa mkoa wetu,uku akihiomba bank hiyo kutazama namna ya kuwawezesha wafanyabiashara.
” Inashangaza sana bidhaa zinazalishwa mkoa wa pwani zinapelekwa Dar- es- salam kwenda kuhuzwa na baadae zinaludi mkoa wa pwani tena kitendo ambacho kinapeleka kodi kuongezeka mkoa wa Dar- es- Salam na si mkoa wa pwani ambapo bidhaa hiyo inazalishwa” Amesema Ndauka.


Pia Ndauka ameeleza swala la kucheleweshwa KWa mikopo imekuwa changamoto KWa wafanyabiashara na kupelekea mtu kupata mkopo wakati husio stahili, Hivyo ameiyomba Benki ya NBC kutazama vyema swala Ilo, pamoja na kuwa wavumilivu na kuangalia namna ya urejeshaji mkopo KWa mkopaji pindi yatokeapo majanga ya kitaifa yanayoweza kusababisha mkopaji kurejesha mkopo.
” Mkopo wa haraka unachukua muda mrefu kupatikana  hasa pale mfanyabiashara anapochukua tenda za kibiashara wanaitaji kulipa KWa ajiri ya kufanikisha tenda haliyo chukua Mwisho wa siku anajikuta anapata mkopo wakati muda wa kufanikisha hiyo tenda aliyopata umekwisha” Amesema Ndauka.


Kwa upande wake Meneja wa la tawi la NBC mkoa wa pwani Baraka Ndandala amewataka wafanyabiashara waje wachukue mikopo na wapo tayali kutazama taarifa za mfanyabiashara kutoka bank zingine Ili Kurahisisha mfanyabiashara kupata mkopo anahohitaji.


Ndandala  ameeleza kuwa bank hitakuwa wawazi KWa mkopaji kabla ya  mkopaji kukopa mkopo huo, uku akifafanua swala la dhamana KWa mkopaji yameboresha tofauti na mwanzo, sasa unaweza kukopeshwa hata husipokuwa na dhamana ya hati kulingana na kiwango cha mkopaji.

.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »