UBORA WA KOROSHO UMEONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 95 HADI KUFIKIA ASILIMIA 97

UBORA WA KOROSHO UMEONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 95 HADI KUFIKIA ASILIMIA 97

Na Moreen Rojas Dodoma Jumla ya tani 8,959.023 za korosho ghafi zilibanguliwa ndani ya nchi kati ya tani 240,158.753 zilizozalishwa sawa na 3.7% na jumla ya leseni 55 za ununuzi wa korosho kwa ajili ya kusafishia nje ya nchi zilizotolewa ikiwa ni ongezeko la kampuni 5 ukilinganisha na leseni katika msimu wa 2020/2021. Fransis Afred

Na Moreen Rojas Dodoma


Jumla ya tani 8,959.023 za korosho ghafi zilibanguliwa ndani ya nchi kati ya tani 240,158.753 zilizozalishwa sawa na 3.7% na jumla ya leseni 55 za ununuzi wa korosho kwa ajili ya kusafishia nje ya nchi zilizotolewa ikiwa ni ongezeko la kampuni 5 ukilinganisha na leseni katika msimu wa 2020/2021.


Fransis Afred ni Mkurugenzi wa bodi ya Korosho amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma lengo ni kutoa taarifa ya itekelezaji wa shughuli mbalimbali za bodi hiyo kwa mwaka 2021/2022 na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2022/2023.


Aidha ameongeza kuwa kiasi cha kilo 91,764 za mbegu bora za korosho zenye thamani ya shilingi 275,292,000 zimesambazwa katika halmashauri 87 zinazolima korosho hapa  nchini ikiwa ni mkakati mojawapo wa kufikia uzalishaji wa korosho ghafi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/2026.


Wakulima 281,200 walisajiliwa kati ya wakulima 318,407 waliotarajiwa kusajiliwa sawa na 88% jumla ya wakulima na wapuliziaji 1,304, Viongozi wa Amcos 703 pamoja na maafisa ugani 1,923 wamepatiwa mafunzo bora ya kilimo cha korosho kwa kushirikiana na Tari _Naliendele “Amesema Afred.


Pikipiki 95 zenye thamani ya shilingi 297,514,236 zilizotolewa kwa maafisa ugani ikiwa ni nyezo muhimu katika kuwafikia na kuwahudumia wakulima kwa wakati.


Pamoja na hayo jumla ya maafisa ugani 536 kutoka mikoa ya Mtwara,Lindi,Ruvuma,Pwani na Tanga waliweza kunufaika na mpango wa motisha ya shilingi 100,000 kwa mwezi juu ya utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima takribani shilingi milioni 200 zilitengwa kwa ajili hiyo.


Kiasi cha tani 30,000 kinatarajiwa kubanguliwa hapa nchini kati ya tani 400,000 zinazotarajiwa kuzalishwa,jumla ya leseni 60 zinatarajiwa kutolewa kwa msimu huu ambapo hadi sasa jumla ya kampuni 25 zimewasilisha maombi ya leseni ” Amesema Afred.
Bodi ya Korosho Tanzania inaendelea na maandalizi ya usimamizi wa masoko na mauzo ya korosho ghafi ili kuhakikisha msimu wa mwaka 2022/2023 unakuwa na mafanikio kwa wadau wa Tasnia ya korosho nchini.
Bodi tayari imeanza kusajili na kutoa leseni kwa wanunuzi wa korosho ghafi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na kubangua nchini ambapo hadi kufukia tarehe 07 oktoba 2022,jumla ya kampuni 48 zimesajiliwa na kati yake kampuni 18 tayari zimepata leseni na zilizosalia zipo katika hatua mbalimbali za kukamilisha upatikanaji wa leseni “Amesema Afred.
 Bodi itaendelea kushirikina na wadau wote katika mnyororo wa zao la korosho kuhakikisha mkulima anazalisha na kuuza korosho zake kwa tija kwa maendeleo ya tasnia ya korosho nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »