WANANCHI WAHIMIZWA KUJIUNGA NA PROGRAM ZA ELIMU YA WATU WAZIMA

WANANCHI WAHIMIZWA KUJIUNGA NA PROGRAM ZA ELIMU YA WATU WAZIMA

Na.Moreen Rojas, Dodoma. Taasisi ya Elimu ya watu wazima( TEWW) imetoa wito Kwa wananchi kujiunga na program za elimu ya watu wazima kwani inatoa elimu kwa nadharia na vitendo kwa kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuwa mtu bora mwenye uwezo wa kujiendeleza na kupambana na changamoto za maisha. Hayo yamesemwa na mkurugezi wa taasisi ya Elimu

Na.Moreen Rojas, Dodoma.

Taasisi ya Elimu ya watu wazima( TEWW) imetoa wito Kwa wananchi kujiunga na program za elimu ya watu wazima kwani inatoa elimu kwa nadharia na vitendo kwa kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuwa mtu bora mwenye uwezo wa kujiendeleza na kupambana na changamoto za maisha.

Hayo yamesemwa na mkurugezi wa taasisi ya Elimu ya watu wazima  Dkt. Michael Ngumbi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Juu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi ya Elimu ya watu wazima (TEWW) pamoja na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema taasisi imeongeza wigo wa kutoa elimu kulingana na uhitaji wa elimu ya watu wazima nchini na imekuwa na mchango chanya ambayo inamuwezesha mtu mzima kutatua changamoto za maisha katika mazingira anayoishi.

Aidha amesema kuwa jumla ya Billion 15 na million 531 zimetegwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023  ikiwa ni Ongezeko la 7.2% ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2021/2022 katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za taasisi ya Elimu ya watu wazima.

Taasisi ya elimu ya watu wazima ni taasisi ya umma iliyoanzishwa chini ya wizara ya elimu , sayansi na teknolojia kwa lengo la kutoa na kusimamia elimu  ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »