TSC YAWATAKA WALIMU KUENDELEA KUZINGATIA MIIKO NA MAADILI YA KAZI ZAO 

TSC YAWATAKA WALIMU KUENDELEA KUZINGATIA MIIKO NA MAADILI YA KAZI ZAO 

Na Moreen Rojasi Dodoma Tume ya utumishi wa walimu imewataka walimu kuzingatia miiko na maadili ya kazi zao na kutekeleza majukumu kwa weledi ili kuleta ubora wa elimu hapa nchini. Katibu Mkuu wa Tume ya utumishi wa Walimu Mwalimu Paulina Nkwama amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa


Na Moreen Rojasi Dodoma


Tume ya utumishi wa walimu imewataka walimu kuzingatia miiko na maadili ya kazi zao na kutekeleza majukumu kwa weledi ili kuleta ubora wa elimu hapa nchini.


Katibu Mkuu wa Tume ya utumishi wa Walimu Mwalimu Paulina Nkwama amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.


Mwalimu Nkwama Amesema walimu wasiozingatia maadili ya kazi yao huilazimu TSC kuwafikisha kwenye mamlaka zao za nidhamu kwa mujibu wa kanuni kwaajili ya kushughulikiwa kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili kuwanusuru watoto na kuwafanya wapate huduma inayokusudiwa.


Aidha amesema kuwa chombo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa walimu ili wafanye kazi yao kwa kuzingatia maadili huku akisema pamoja na jitihada hizo lakini bado kuna walimu ambao wamekuwa hawazingatii miiko na maadili ya kazi yao.


“Tume hii imejikita zaidi katika kutoa elimu ili kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu ambapo watendaji wa wilaya wamekuwa wakifika shuleni kutoa elimu kwa walimu pamoja na maadili na kujiepusha na makosa ya kinidhamu kwa walimu”Amesema Mwalimu Nkwama.


Katibu Mkuu Mwalimu Nkwama Amesema  walimu 1,952 walifunguliwa mashauri ya kinidhamu katika mashauri yaliyofunguliwa 1,362 sawa na asilimia 69.8 ya mashauri yote yaliyohusu kughushi vyeti,mashauri 119 sawa na asilimia 6.1 yaliyohusu mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi,mashauri 98 sawa na asilimia 5 yaliyohusu ukaidi,mashauri 66 sawa na asilimia 3.4 yaliyohusu ulevi,mashauri 16 sawa na asilimia 0.8 yaliyohusu ubadhirifu na mashauri 31 sawa na asilimia 1.6 yaliyohusu makosa mengineyo.
“Naomba nisisitize kuwa TSC ni chombo chenu kimeundwa kuwahudumia hakipo kwa ajili ya kuwafukuza kazi walimu la hasha,bali kimeundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kuwahudumia walimu katika ajira zao maadili ya utumishi wao kwa kuhakikisha kwamba walimu wanafanya kazi zao kwa kuzingatia miiko ya maadili ya kazi ya ualimu na maendeleo yao katika utumishi wa umma” Amesisitiza Mwalimu Nkwama.


Pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuwapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa elimu kwa watoto hapa nchini huku akiwasihi kwamba TSC ipo pamoja nao kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »