Na Barnabas Kisengi-Dodoma MKUU wa Mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE ameshiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Bi NEEMA FARAJA SAMWELI iliyofanyika Nyumbani kwao Ilazo Jijini Dodoma. Marehemu NEEMA FARAJA SAMWELI alizaliwa Oktoba 26 Mwaka 1994 na Alifariki Dunia Novemba 06 2022 kwa ajali ya ndege Mkoani kagera ambapo mazishi yake yamefanyika November 09 2022 Jijini
Na Barnabas Kisengi-Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE ameshiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Bi NEEMA FARAJA SAMWELI iliyofanyika Nyumbani kwao Ilazo Jijini Dodoma.

Marehemu NEEMA FARAJA SAMWELI alizaliwa Oktoba 26 Mwaka 1994 na Alifariki Dunia Novemba 06 2022 kwa ajali ya ndege Mkoani kagera ambapo mazishi yake yamefanyika November 09 2022 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameshiriki ibada ya mazishi na kuwapa pole Familia ya Marehemu akiwemo mume wa Marehemu,wazazi na ndugu wa Marehemu Kwa kupatwa na msiba huo.
“Nafahamu watanzania wengi tumeumia na msiba huu lakini kama mnavyo fahamu kuwa RAIS SAMIA SULUH HASSAN alitoa maelekezo tuhakikishe tunashirikiana kuhakikisha tunaipumzisha wenzetu walio tangulia mbele za haki ndio maana nami nipo hapa kuwakikisha Serikali kama tulivyo elekezwa na Mhe RAIS hivyo nawapa pole nyingi sana wazazi na mume wake kwa msiba mzito huu ulio wakuta kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kuwaombea katika sala zetu za kila siku”alisema SENYAMULE.
Mkuu wa wa Mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE Ametoa pole nyingi kwa shirika la MDH kwa kuwapoteza wafanyakazi wengi katika ajali hiyo ya ndege na amesema shirika la MDH limekuwa likishirikiana kufanya kazi Mbalimbali za Afya hapa nchini.
Aidha SENYAMULE amesema kuwa kwa Mkoa wa Dodoma wameguswa na misiba hiyo miwili jana tulikuwa kondoa kumzika Mwenzetu na leo tuko hapa kwa kumzika Marehemu NEEMA FARAJA SAMWELI kama tulivyo elekezwa kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja hivyo kama Serikali tumekuja na ubani wetu walau kidogo wa kuwashika mkono wa pole familia na mume wa Marehemu.
Ikumbukwe kuwa ajali ya Ndege ya shirika la Precision Air ilitokea Jumapili asubuhi majira ya saa mbili katika ziwa Victoria Bukoba Mkoani kagera na kusababisha vifo vya watu 23 na walio okolewa 26
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *