SERIKALI YATOA TSH. BILIONI 6.7 KUKAMILISHA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA JIJINI DODOMA

SERIKALI YATOA TSH. BILIONI 6.7 KUKAMILISHA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA JIJINI DODOMA

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari unaendelea kujengwa jijini Dodoma.Madarasa hayo yanayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kukidhi nafasi kwa wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza wanaotarajia kuanza masomo yao mwakaka 2023. Mkoa wa Dododma Rosemary Senyamule

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari unaendelea kujengwa jijini Dodoma.
Madarasa hayo yanayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kukidhi nafasi kwa wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza wanaotarajia kuanza masomo yao mwakaka 2023.


Mkoa wa Dododma Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma umepokea kiasi cha Tsh.Bilioni 6,780,000,000. kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 339, katika shule za secondary 127, zilizopo katika halmashauri 8 za Mkoa Dodoma.
Senyamule amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi unaendelea katika baadhi ya shule za secondary za Halimashauri ya Jiji la Dodoma amekagua Ujenzi Katika shule ya secondary ya Mnadani na secondary ya Zuzu ambapo shule hizo zinaendelea na Ujenzi wa vyumba viwili viwili na ameona hatua waliyafikia ni kuezeka na kumaliza kupiga lipu Majengo ya vyumba hivyo vya madarasa ikiwa ni hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa Ujenzi huo.


Senyamule akiwa katika shule ya sekondari Zuzu, amewataka wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo kusimamia mradi huo vizuri na umalizike kwa wakati huku akiwataka kamati za Ujenzi kuhakikisha wanaisimamia kila hatua na kutanguliza uzalendo.

“Napenda kuwaambea kuwa Hakikisheni mnamaliza kazi hii ya Ujenzi vizuri na kwa ubora na wakati kwakuwa Mhe  Rais ametoa fedha shilingi Bilioni 6.780 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 339 kwenye shule mbalimbali za mkoa wa Dodoma hivyo  Tuna jukumu la kusimamia fedha hizi zitumike ipasavyo na kwa uzalendo mkubwa”Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Senyamule
“Nafahamu kuwa Mradi hii ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa ilianza Oktoba 10 mwaka huu hadi sasa shule nyingi zimefikia hatua ya upauaji, kuweka kenchi, plasta, madirisha na milango hivyo natarajia hadi kufikia  Novemba 20 miradi hii yote ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Mkoa wa Dodoma vitakuwa vimekamilika”Alisisitiza Senyamule


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma anaendelea na ziara yake ya ukaguzi wa Ujenzi wa vyumba vya madarasa 339 vya madarasa ya secondary vinavyoendelea kujengwa katika Halimashauri 8 za Mkoa wa Dodoma.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »