WANAFUNZI WA KIKE WANAONGOZA KWENYE UDAHILI(TICD).

WANAFUNZI WA KIKE WANAONGOZA KWENYE UDAHILI(TICD).

Na Moreen Rojas Dodoma Kwa mwaka 2021/2022, taasisi ilikuwa na jumla ya wanafunzi 2749 kati ya hao,wanafunzi 1812 sawa na 65.9% walikuwa ni wanawake na wanafunzi 935 sawa na 34.1% walikuwa ni wanaume,hili ni ongezeko la wanafunzi 139 sawa na 5.3% ya idadi ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/2021. Dkt.Bakari George Mkuu wa Taasisi


Na Moreen Rojas Dodoma


Kwa mwaka 2021/2022, taasisi ilikuwa na jumla ya wanafunzi 2749 kati ya hao,wanafunzi 1812 sawa na 65.9% walikuwa ni wanawake na wanafunzi 935 sawa na 34.1% walikuwa ni wanaume,hili ni ongezeko la wanafunzi 139 sawa na 5.3% ya idadi ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/2021.


Dkt.Bakari George Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya jamii Tengeru(TICD) amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma kueleza utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo na vipaumbele kwa mwaka 2022/23.


Amesema kwa namna ya pekee kukamilika kwa mradi wa hosteli ya wasichana licha ya kuwa utapunguza sana changamoto ya malazi iliyokuwa inakabili wasichana na kuimarisha mifumo ya uangalizi wa malezi,mradi huu unakwenda kuongeza wigo wa vyanzo vya mapato kwa taasisi ambapo kiasi cha shilingi 187,440,000.00 kinatarajiwa kukusanywa kwa mwaka kutokana na ada ya malipo ya hosteli kwa wanafunzi watakaopangiwa hosteli.
“Sababu nyingine ya kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi ni upatikanaji wa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu ( HESLB) mathalani kwa mwaka 2021/2022 wanafunzi 448 walipata jumla ya shilingi 1,153,376,000.00 na kwa mwaka 2022/2023 idadi ya wanufaika wa mikopo inatarajiwa kuwa 450 watakaopata jumla ya shilingi 1,158,525,000.00″Amesema Dkt.Bakari.


Aidha taasisi imeendelea na jitihada za kuwajengea uwezo watumishi wake ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/2022,taasisi ilitumia kiasi cha shilingi 183,978,000.00 kugharamia mafunzo kwa watumishi 27 katika ngazi ya shahada za awali,uzamili na uzamivu na mafunzo mengine ya muda mfupi.


Kwa mwaka 2022/2023 taasisi imetenga kiasi cha shilingi 245,133,000.00 kimetegwa kwa ajili ya kuwagharamia watumishi wapatao 31 ambao watajiunga na taasisi mbalimbali za elimu hapa nchini.


Aidha kituo kwa kushirikiana na wadau wapatao 53 yakiwemo mashirika,taasisi za kifedha,taasisi za serikali,wahitimu wapatao 108 kati yao ni wanawake wakiwa 66 na wanaume wakiwa 42 waliweza kupata ujuzi mbalimbali ambao uliwasaidia wahitimu 86 kuajiriwa na taasisi mbalimbali na wahitimu 22 kujiajiri.


Aidha ameongeza kuwa kwa mwaka 2021/22 taasisi katika utekelezaji wa shughuli za michezo imekuwa ikitenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha washiriki 40 kushiriki mashindano ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimu ya juu Tanzania ( SHIMIVUTA) mkoani Iringa ambapo timu ya mpira wa miguu kutoka taasisi hii ilikuwa mshindi wa pili kitaifa na hivyo kuzawadiwa kombe,aidha watumishi 35 waliweza kushiriki mashindano ya shirikisho la michezo la mashirika ya umma na makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) huko Morogoro.


Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 taasisi imepanga kuanzisha mradi wa tofali mradi ambao utaongeza ajira kwa wanajamii na wanafunzi wenye utayari pamoja na kuwawezesha watumishi kujenga na kuboresha makazi yao kwa gharama rahisi na viwango vizuri kulinganisha na ilivyo sokoni,mradi mwingine utakaoanzishwa ni wa ufugaji wa samaki.


Mkurugenzi mkuu wa habari maelezo na Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa ameipongeza taasisi hiyo na kusema kuwa serikali kwa kutambua mchango wa taaaasisi hiyo imeajiri zaidi ya maafisa wa maendeleo ya jamii 3000 kwani umuhimu wao kwenye jamii ni mkubwa kwa ajili ya kuweza kuhamasisha mambo mbalimbali kwani ni kazi inayoheshimika kwenye jamii.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »