WAGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WAPUNGUA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

WAGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WAPUNGUA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

Na. Wellu Mtaki, Dodoma Daktari Bingwa ya magonjwa ya wanawake katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dr. Enid Chiwanga Amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi  wanaofika kupata matibabu imepungua ikilinganishwa na miaka michache iliyopita. Ameyasema hayo leo November 14 2022 alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Mwandishi wa hahari 

Na. Wellu Mtaki, Dodoma


Daktari Bingwa ya magonjwa ya wanawake katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dr. Enid Chiwanga Amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi  wanaofika kupata matibabu imepungua ikilinganishwa na miaka michache iliyopita.


Ameyasema hayo leo November 14 2022 alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Mwandishi wa hahari  wa J five One line blog ofisini kwake Juu ya tatizo ya saratani ya shingo ya kikazi katika mkoa wa dodoma.
Dr. Chiwanga Amesema kuwa ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi bado Upo lakini kwa sasa ni tofauti na miaka iliyopita KWa kuwa wanapokea wagonjwa wachache wanaofanyiwa uchunguzi ili kubaini tatizo ilo.


Aidha amefafanua kuwa elimu bado inaitajika KWa jamiii ili kuwasaidia wakina mama ambao wanaoatwa na ugonjwa huu waweze kupata uchunguzi na matibabu kwa kuwa wakina mama wengi wanaofika hospital wanakuwa katika  hali mbaya hali ambayo inahatarisha maisha yao.


Pia Dr Chiwanga ametoa wito kwa wataalamu wa afya kuwasisitiza wanawake wanapofika Kwenye vituo vyao afya au hospital wawape ushauri wa kujenga utamaduni wa kupima salatani ya shingo ya kizazi mara KWa mara.


Ametaja baadhi ya dalili ya salatani hiyo ni pamoja na kutokwa na damu pale wanaposhiriki tendo la ndoa na mwezi wake, mwanamke kupata hedhi hisiyokuwa na mpangilio pamoja na kutokwa majimaji ukeni wenye harufu kali.
.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »