RC MAKALLA AMSHUKURU RAIS SAMIA KUTOA BILIONI 3 UJENZI SHULE MPYA YA WASICHANA DSM

RC MAKALLA AMSHUKURU RAIS SAMIA KUTOA BILIONI 3 UJENZI SHULE MPYA YA WASICHANA DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Shule Mpya ya wasichana Dar es salaam inayojengwa kwenye Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo ambapo amemshukuru Rais Samia kwa kutoa Shilingi Bilioni 3 za kufanikisha Ujenzi huo. RC Makalla amesema Shule hiyo ya bweni itachukuwa Wanafunzi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Shule Mpya ya wasichana Dar es salaam inayojengwa kwenye Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo ambapo amemshukuru Rais Samia kwa kutoa Shilingi Bilioni 3 za kufanikisha Ujenzi huo.

RC Makalla amesema Shule hiyo ya bweni itachukuwa Wanafunzi kuanzia kidato Cha kwanza mpaka kidato Cha sita.

Katika ziara hiyo RC Makalla amepokea taarifa ya mwenendo wa Ujenzi huo ambao kwa mujibu wa Mkandarasi Ujenzi utakamilika na kukabidhiwa mwezi Disemba mwaka huu.

Aidha RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Ubungo kuanza maandalizi ya kuweka eneo la Shule kwenye Hali nzuri ikiwemo Ujenzi wa uzio, vigae kwenye sehemu za watembea kwa miguu na upandaji maua na miti ya kivuli.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »