TANZANIA MIONGONI MWA NCHI 5 UTEKELEZAJI WA KUKABILIANA NA DHARURA NA MAJANGA AFRIKA

TANZANIA MIONGONI MWA NCHI 5 UTEKELEZAJI WA KUKABILIANA NA DHARURA NA MAJANGA AFRIKA

Na. Catherine Sungura, Wizara ya Afya-Dodoma Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 kati ya 17 za awamu ya kwanza barani Afrika  zitakazotekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wa sekta ya afya kujiandaa, kugundua na kukabiliana na dharura na majanga. Wataalamu wa sekta ya mbalimbali wanaoshirikiana na sekta ya afya katika  kukabiliana na dharura na majanga wameshiriki. 

Na. Catherine Sungura, Wizara ya Afya-Dodoma


Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 kati ya 17 za awamu ya kwanza barani Afrika  zitakazotekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wa sekta ya afya kujiandaa, kugundua na kukabiliana na dharura na majanga.

Wataalamu wa sekta ya mbalimbali wanaoshirikiana na sekta ya afya katika  kukabiliana na dharura na majanga wameshiriki.  Mradi umepanga kuendeleza kutumia mifumo na juhudi zilizopo na kuboresha zaidi. Hii itahusisha ushirikiano na sekta mbalimbali katika kufikia utayari wa kukabiliana na matukio ya dharura na majanga.


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo wakati wa kufungua mkutano kujadili namna bora ya utekelezaji wa mradi huo. Mkutano umewajumuisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali nchini unaofanyika jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa katika mradi huo unaojulikana kama “Flagship Initiative”  utaisaidia nchi  kuwa na mfumo sahihi wa kukabiliana na dharura na majanga  kwa kuimarisha mpango kazi  wa uwezo wa kujiandaa, kugundua na kukabiliana na dharura na majanga pamoja na kujizatiti katika kuimarisha mipango yao.
“Tunashukuru kwamba tunakuwa  kati ya nchi tano (5) za Afrika ambazo zitaanza kufaidika kutekeleza  Mradi huu, tunaamini tutafanikiwa kujengewa uwezo wetu wa kuandaa, kugundua na kukabiliana na dharura za afya kwa jamii na kuwezesha kujenga miundombinu iliyopo na kuweka mifumo sahihi itakayosaidia kuongeza uwezo wa Kitaifa katika kujiandaa kukabiliana na dharura na maafa”.amesema Waziri Ummy.


Waziri ummy amesema kuwa hivi sasa nchi imekua ikikumbwa na majanga mbalimbali pamoja na  dharura  na wakati mwingine wanapata changamoto kwa kukosa mfumo imara wa afya wa kukabiliana na changamoto hizo.Akitolea mfano  wakati wa janga la UVIKO-19  amesema kuwa wamejifunza kwa kuimarisha mfumo wa dharura ikiwemo huduma za hewa ya Oksjeni na hatua hiyo imefanya sekta ya afya kufunga mifumo ya hewa tiba kuanzia hospitali ya taifa, kanda, hospitali za Rufaa za Mikoam rufaa pamoja na baadhi ya hospitali za Halmashauri.
“Janga la UVIKO-19 pia imetufundisha kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana na sekta mbalimbali na hivyo tuliweza kuratibu kama sekta na sasa tunaangalia mbele katika utayari wa kukabiliana na maafa na majanga nchini” Amesisitiza Waziri Ummy.


Aidha, Waziri Ummy amesema Magonjwa mengi ya milipuko yanayowapata binadamu yanatoka kwa wanyama  kwa hivyo ushirikiano wa sekta mbalimbali ni muhimu katika kujitayarisha kukabiliana na magonjwa ya milipuko kwani hata mabadiliko ya tabia nchi nayo yanachangia pia kuibuka kwa magonjwa yanayoathiri afya ya jamii.


Amesema utekelezaji wa mradi huo unalenga  kwa pamoja kuboresha uwezo wa nchi wanachama kujiandaa, kugundua na kukabiliana  na magonjwa ya milipuko yanayoathiri afya ya jamii na hivyo ameishukuru WHO Afrika kwa mafunzo ya  kuwajengea uwezo wataalamu wa sekata mbalimbali hapa nchini.
“Mafunzo haya yamekuja wakati sahihi na itatusaidia kuangalia utayari wetu na tunaishukuru WHO kwa kuendelea kusapoti Serikali hususani katika utayari wa kukabiliana na dharura na majanga nchini, na kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama, tunaahidi ushirikiano katika kutekeleza mradi huu kwa kushirikiana na sekta nyingine”amesema Waziri Ummy
Akiongea katika mkutano huo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya duniani nchini Tanzania (WHO ) Dkt. Zabron Yoti amesema asilimia 70 ya magonjwa ya milipuko yanayowapata binadamu yanatoka kwa wanyama hivyo  usalama wa afya ni kipaumbele cha dunia na kama nchi inahitaji kujengewa uelewa kwa kushirikisha sekta zote.


Amesema  ni vyema kuwalinda wananchi na dharura na majanga kwani mabadiliko ya tabia nchi nayo huchangia magonjwa ya milipuko.
“Ni vyema kujiandaa mapema  kwani kutojiandaa ni hatari na hivyo kama WHO  wapo tayari kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko yakiwemo yanayotokana na wanyama.
Naye, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Edward Mbanga amewashukuru WHO kuwa washirikia wazuri wa kuisadia serikali ya Tanzania kwani hivi sasa tunaishi dunia yenye dharura hivyo hatuwezi kuzuia yasitokee ila ni vyema kujiweka tayari katika kukabiliana nayo.


Nchi nyingine zitakazotekeleza mradi huo ni Botswana, Mauritania, Niger,Nigeria,Togo,Chad,Congo, DRC  pamoja na nyinginezo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »