Waumini Kanisa la Moravian Tanzania watakiwa kutochoka kuwasaidia Wenye uhitaji.

Waumini Kanisa la Moravian Tanzania watakiwa kutochoka kuwasaidia Wenye uhitaji.

Na, Emesto Eliudy, Dar Es Salaam. Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Limewataka waumini wa Kanisa Hilo na watanzania Kwa ujumla kutochoka kuwasaidia watu waishio katika mazingira Magumu ikiwa ni sehemu Yao ya Ibada Kwa Mungu. Kauli hiyo ilitolewa asubuhi ya Leo Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Kanisa Hilo Jimbo la Mashariki,

Na, Emesto Eliudy, Dar Es Salaam.


Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Limewataka waumini wa Kanisa Hilo na watanzania Kwa ujumla kutochoka kuwasaidia watu waishio katika mazingira Magumu ikiwa ni sehemu Yao ya Ibada Kwa Mungu.


Kauli hiyo ilitolewa asubuhi ya Leo Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Kanisa Hilo Jimbo la Mashariki, Mch. Gerhard Simtengu wakati akikabidhi Mahitaji Mbalimbali Katika Shule ya watoto wenye Ulemavu iliyopo ndani ya kituo Cha Jeshi la Wokovu kilichopo Temeke Jijini Dar Es Salaam ambapo alisema Kuwa kufanya hivyo ni sehemu Kubwa ya Ibada ambayo inampendeza Mungu.

Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki, Mch. Gerhard Simtengu. (Picha na Emesto Eliudy)


“Nitumie nafasi hii kuwaomba wamoravian Wenzetu kwamba tusiache kufanya huduma kama hii, mbali na kituo hiki Cha Jeshi la Wokovu, tunao watu Maalum ambao wanahitaji Sana msaada wetu. Tunahitaji hata kwenye Shirika zetu, kwenye Wilaya zetu na kwenye maeneo yetu ya Misheni kuendeleza huduma hii bila kuchoka”.Alisema Mch. Simtengu.


Aidha Mch. Simtengu alimuagiza Katibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii ya Kanisa Hilo Jimbo la Mashariki, Mch. Suma Mwankuga kushirikiana na makatibu wa Idara hiyo katika Shirika mbalimbali kuweka mpango Maalumu wa Kuendeleza huduma hiyo ikiwemo kufungua kituo Maalumu Cha kulelea watoto waishio Katika mazingira hatarishi.


“Namhimiza Katibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii kushirikiana na makatibu wa Idara hiyo ngazi ya Ushirika kuweka mpango Maalumu wa Kuendeleza huduma hii. Naamini tayari ameleta mpango wa kuwa na kituo kama Kanisa ambacho tutashughulika nacho lakini kabla ya kumiliki kituo chetu, hudumu hii ambayo imefanyika hapa iendelezwe ndani ya Kanisa la Moravian”. Alisema Mch. Simtengu.

Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Ya kanisa hilo Jimbo la Mashariki, Mch. Suma Mwankuga, alisema Kuwa Kanisa liliguswa kutoa sadaka hiyo kwasababu watoto wanastahili kuhudumiwa Kibiblia.

Katibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki, Mch. Suma Mwankuga. (Picha na Emesto Eliudy)


” Kama Kanisa tuliguswa kuwa na sadaka hii ya kufanya tendo hili kwasababu watoto Hawa wanastahili kuhudumiwa na sisi Kibiblia sawa na Mithali 19:17. kwahiyo sisi kama Kanisa ni sehemu yetu kuwahurumia au kuwahudumia Wahitaji na miongoni mwa wahitaji ni Pamoja na watoto ambao wapo mahali hapa”. Alisema Mch. Suma.


Pia Mch. Suma alizitaka Jamii na taasisi Mbalimbali kuwa na utayari wa kutoa sadaka Kwa ajili ya wahitaji ili ziweze kupokea Baraka Kwa Mungu.


“Nitoe wito Kwa Jamii na taasisi zote kuwa ni Muhimu Sana kuwatazama wahitaji wa aina mbalimbali, hivyo ni Vizuri kutoa sadaka Kwa ajili ya wahitaji ili tuweze kuzipokea Baraka kutoka Kwa Mungu lakini pia tuweze kuwajibika maana ni wajibu wetu kufanya Haya” aliongeza Mch. Suma.

Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki, Mch. Gerhard Simtengu akikabidhi kiloba cha Unga kwa Mkurugenzi wa Shule ya Walemavu katika kituo cha Jeshi la Wokovu, Kapteni Jackson Nyamhanga. (Picha na Emesto Eliudy)

Naye Mkurugenzi wa Shule hiyo, Kapteni Jackson Nyamhanga alisema Kuwa kituo hicho kina idadi ya jumla ya watoto 236 ambapo Kila Darasa linachukua watoto 30 huku wengine wakihamia kutoka shule Mbalimbali kutokana na Baadhi ya watoto wenzao kuwacheka.

Mkurugenzi wa Shule ya Walemavu katika kituo cha Jeshi la Wokovu, Kapteni Jackson Nyamhanga akiwatambulisha wageni kutoka kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki walipotembelea katika kituo hicho asubuhi ya leo. (Picha na Emesto Eliudy)


“kituo hiki kina idadi ya watoto 236 na Kila Darasa tunachukua watoto 30 lakini pia wapo ambao wanahamia kutoka shule zingine kwasababu Mtoto mwenye Ulemavu anapokua katika Shule hizo anaonekana kama sio sehemu yake na watoto wenzake wanampuuza na kumcheka ndiyo maana wanahamia hapa na tunawapokea na wanaendelea kupata Elimu katika Shule Yetu”. Alisema Kapteni Nyamhanga.

Katibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki, Mch. Suma Mwankuga pamoja na Mwenyekiti wa Kanisa hilo Jimbo la Mashariki, Mch. Gerhard Simtengu wakikabidhi Sabuni kwa Mkurugenzi wa Shule ya Walemavu, Kapteni Jackson Nyamhanga. (Picha na Emesto Eliudy)


Aidha Kapteni Nyamhanga alilishukuru Kanisa la Moravian Kwa sadaka Yao huku akitoa wito Kwa Watanzania kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye Ulemavu badala yake wapeleke shuleni hapo ili wakapate Elimu maana ni haki yao na pia wafahamu kuwa Mtoto mlemavu siyo mkosi kwenye familia. 


“Tunalishukuru Kanisa la Moravian Kwa Namna ambavyo wamefikiria kuja Kwa ajili ya watoto hawa, tunaliombea Kanisa Hilo Mungu aendelee kuonekana katika Maisha yao”.


“Wito wangu Kwa watu wenye watoto wenye ulemavu wasiwaweke tu nyumbani ni muhimu Sana na ni haki ya Kila Mtoto kupata Elimu. Shule hii ipo Kwa ajili ya watoto wote wenye Ulemavu Katika Mikoa Mbalimbali Tanzania, Kila Mkoa una mwakilishi wa Mtoto hapa” alisema Kapteni Nyamhanga.

Sadaka zilizotolewa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki katika Shule ya Walemavu iliyopo kaika kituo cha Jeshi la Wokovu kilichopo Temeke Jijini Dar Es Salaam. (Picha na Emesto Eliudy)


” Wengi wanafikiria kwamba Mtoto mwenye Ulemavu anapozaliwa kwenye familia wengi wanadhani ameleta mkosi na laana, siyo hivyo, huu ni mpango wa Mungu ambao anafanya mwenyewe akimaanisha katika Maisha ya kila Mtu ” aliongeza Kapteni Nyamhanga. 

ReplyForward
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »