WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI

Na Moreen Rojas-Dodoma Mkurugenzi wa kampuni ya Cornwell Tanzania na Daktari wa Tiba Asili Daktari Elizabeth Lema amewahimiza watanzania kutumia dawa za asili na kuwashauri wananchi wanapotafuta tiba waanze kufikiri dawa za kitanzania. Dk.Elizabethi ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na mwandishi wa J five One line blog katika ukumbi wa Jakaya Convention Jijini Dodoma

Na Moreen Rojas-Dodoma


Mkurugenzi wa kampuni ya Cornwell Tanzania na Daktari wa Tiba Asili Daktari Elizabeth Lema amewahimiza watanzania kutumia dawa za asili na kuwashauri wananchi wanapotafuta tiba waanze kufikiri dawa za kitanzania.


Dk.Elizabethi ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na mwandishi wa J five One line blog katika ukumbi wa Jakaya Convention Jijini Dodoma ambapo Kuna mkutano wa wataalam wa dawa Tanzania.

Amesema kuwa watanzania na waafrika tuna dawa za asili na virutubisho lakini hatujazipeleka na kuonyesha zina fanyakazi kwa uzuri kiasi gani,kwahiyo kampuni hiyo wanatengeneza kwa njia ya vidonge.
“Tunatengeneza dawa zetu kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia mimea ya kitanzania kwa ajili ya watoto na watu wazima na tumesajiliwa na Tanzania Investment Center kwa sababu sisi ni wawekezaji wa ndani”Amesema Dk.Elizabeth.


Aidha Dk Elizabeth amesema kuwa mpaka sasa wameshasajili dawa nne pamoja na virutubisho na wanaendelea na usajili kwani wana dawa takribani mia moja 100 ambazo zinatokana na mimea ya kitanzania.
“Dawa zetu za asili na mimea yetu ya kitanzania ina uwezo mkubwa sana katika kutibu magonjwa yanayotokana na maisha yetu ya kila siku,mfumo wa maisha,magonjwa ya maambukizi,yote ni sisi kujifunza na kuzielewa”Amesisitiza Dk.Elizabeth.


“Nawashauri watanzania wenzangu kutumia dawa zetu za asili kwani zina virutubisho,kwani tiba yetu inatokana na pale tulipozaliwa kwa sababu tunashirikiana sana na mimea ya hapa na ardhi ya hapa hivyo kila dawa utakayotumia itaweza kukutibu vizuri”
“Amesema ni muda muafaka kwa watanzania na waafrika kuziangalia dawa zetu za asili na kampuni yetu  inaleta bidhaa sokoni kitaalam kabisa na wana madaktari bigwa kabisa nikiwemo Mimi mwenyewe kwa sababu wanaelewa jinsi dawa zinavyofanyakazi pamoja na mwingiliano wa dawa”Amesisitiza Dk Elizabeth
“Wakati mwingine unaweza ukawa unatumia dawa za hospitali tukaangalia pia ni namna gani tunaweza kukupa dawa zetu za asili na zikakusaidia kwa hiyo tunapaswa kuangalia dawa za asili kwani tunaweza kutibu magonjwa yanayotusumbua kwa kutumia dawa za asili”Amesema Dk.Elizabeth 


Pia ameongeza kuwa anawasihi watanzania kutunza miti kwani watu wanakata miti dawa bila kujua ina faida,wanachoma mikaa wanapoteza dawa kukata Kuni kwahiyo nivizuri kabla ya kukata miti ukajua itakupa faida kwa wenye viwanda Kununua na kutengeneza dawa,hivyo tulinde sana miti yetu na mimea yetu ya asili.
“Kwa mfano mimi hapa sasahivi natafuta mizizi ya upupu na iko mikoa ambayo upupu ni mwingi sana kwahiyo ni vizuri kutumia fursa za namna hiyo na kuweza kujipatia pesa,kwani kilo moja ya mizizi ya upupu inanunuliwa kwa bei nzurii sana”Ameongeza Dk.Elizabethi

Aidha Dk.Elizabeth ameishukuru Serikali haswa Mhe.RAIS SAMIA SULUH HASSAN  kwani amekuwa akitoa ushirikiano wa tiba asili na Wizara ya afya kwa kuweza kuwatambua na kupeleka tafiti ya tiba asili na kuandaa tukio la umoja wa wataalam wa dawa Tanzania na kuwatambua wataalam wa dawa za asili tofauti na miaka ya nyuma.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »