WANAWAKE WAASWA KUWA NA TABIA YA KUFANYA UCHUNGUZI MARA KWA MARA ILI KUPATA TIBA YA MAGONJWA YA KIZAZI

WANAWAKE WAASWA KUWA NA TABIA YA KUFANYA UCHUNGUZI MARA KWA MARA ILI KUPATA TIBA YA MAGONJWA YA KIZAZI

Na Moreen Rojas. Dodoma Meneja masoko wa kampuni ya Kasum Helthcare Pvt ltd Dk.Peter Gitau amewaasa wanawake kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa na kupata tiba ya magonjwa ya kizazi ili kulinda vizazi vyao. Dk.Gitau ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Convention ambapo

Na Moreen Rojas. Dodoma


Meneja masoko wa kampuni ya Kasum Helthcare Pvt ltd Dk.Peter Gitau amewaasa wanawake kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa na kupata tiba ya magonjwa ya kizazi ili kulinda vizazi vyao.

Dk.Gitau ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Convention ambapo kuna mkutano wa umoja wa wataalam wa dawa Tanzania.


Amesema kampuni hiyo inafanya uzalishaji wa dawa zaidi ya 100 na wapo katika nchi mbili ambazo zinazalisha dawa ambazo ni Ukraine pamoja na india kwa hapa Tanzania wanaofisi Dar_es_Salaam.
“Tupo hapa Dodoma kwwnye mkutano wa wataalam wa dawa Tanzania lengo letu kubwa ni kuendeleza ufahamu wa dawa tunazungumzia teknolojia mpya ambazo zimejitokeza kwenye dawa mpya ili wataalam waendelee kupata ufahamu zaidi wakutumia dawa za kisasa,dawa ambazo zinatibu kiurahisi ukilinganisha na dawa zingine ambazo zimekuwa zikitumika hapo mwanzoni” Amesema Dk.Gitau

Aidha amesema wana dawa za kina mama kwa sababu magonjwa kama U.T.I ni magonjwa ambayo ni kawaida sana hapa Tanzania na hata mwaka uliopita kulingana na takwimu ambazo zilijitokeza ni kwamba U.T.I ilikuwa ya pili kwa idadi ya wagonjwa waliofika hospitali,kwahiyo wapo kwaajili ya suluhisho la ugonjwa huo.
“Hatuna changamoto yoyote kwasababu taasisi zote za serikali kuanzia T.M.D.A miongozo yao inajieleza vizuri na kila wakati wapo tayari kutupa ushirikiano ndomaaana tumepania kuwa kwenye soko la Tanzania kwa muda mrefu na kuna dawa zingine tunatarajia kuongeza” Amesema Dk.Gitau


Aidha ametoa wito kwa jamii na watanzania wasisubiri sana ugonjwa kuwa mkubwa na badala yake kupata tiba kwa haraka,na pia kuacha kutumia dawa kiholela na badala yake iwe kama ilivyoshauriwa na mtaalam wa afya kwani ukidhurika utatumia gharama kubwa kwenye matibabu kutokana na ugonjwa kuwa sugu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »