MKURUGENZI HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA AKUTANA NA MABALOZI

MKURUGENZI HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA AKUTANA NA MABALOZI

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika November 24 2022 amekutana na mabalozi wa Tanzania waliopo Mashariki ya kati,Ulaya na Amerika, Asia pamoja na Australasia kwa dhumuni la kuwaeleza mafanikio yaliyo letwa na Serikali katika sekta ya afya.”Hospitali ya Benjamin Mkapa ni Hospitali ya Serikali inayo wahudumia wananchi wote kwa kiwango kinacho stahili”amesema Dkt.Chandika  “Serikali

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika November 24 2022 amekutana na mabalozi wa Tanzania waliopo Mashariki ya kati,Ulaya na Amerika, Asia pamoja na Australasia kwa dhumuni la kuwaeleza mafanikio yaliyo letwa na Serikali katika sekta ya afya.”Hospitali ya Benjamin Mkapa ni Hospitali ya Serikali inayo wahudumia wananchi wote kwa kiwango kinacho stahili”amesema Dkt.Chandika 
 “Serikali imewekeza pesa nyingi kwa kuweka majengo mazuri, vifaa tiba vya kisasa na rasilimali watu, hivyo nasi tunatoa huduma kwa viwango hivyo hivyo, tokea Hospitali ianzishwe mahusiano baina ya Hospitali na nchi za nje yamekuwa yakiimarika siku kwa siku”Alisisitiza Dkt Chandika


Kwaupande wake  Balozi Dr Asha Rose Migiro ameipongeza Hospitali kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma zinazoendana na teknolojia ya sasa tena kwakuzingatia huduma kwa mteja. “Ukifika Hospitali ya Benjamin Mkapa huitaji kujitambulisha ili upate huduma nzuri maana utahudumiwa kwa kiwango kizuri pasipo kujali wadhifa wako kwakweli mnastahili pongezi kubwa, endeleeni na moyo huo wa kuwahudumia wananchi pasipo kubagua” amsema Balozi  Dr Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Kwa Upande wake Balozi Swaiba Mndeme ameeleza nimuhimu kuzisaidia Taasisi zetu hususani Hospitali za hapa Nchini

“Tunaposaidia hizi Hospitali hapa Nchini tunakuwa tumewafikia wananchi moja kwa moja nasi tuna kuwa tumefikia shabaha yetu iwe ni kuwasidia wananchi kwa kuiunganisha  na Hospital ya Benjamin Mkapa na wataalamu walipo kwenye nchi tulizopo”amesema Balozi Swahiba.
Hospitali ya Benjamin Mkapa ilizinduliwa Tarehe Oktober 13/2015 toka izinduliwe imekuwa ikikuwa kwa kasi kubwa huku ikitoa huduma zake kwa ubunifu wa hali ya juu na viwango vikubwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »