SERIKALI YATOA UFAFANUZI IDADI NDOGO YA WANAFUNZI KUPANGIWA SHULE ZA BWENI KIDATO CHA KWANZA

SERIKALI YATOA UFAFANUZI IDADI NDOGO YA WANAFUNZI KUPANGIWA SHULE ZA BWENI KIDATO CHA KWANZA

Na Barnabas Kisengi-Kongwa SIKU za hivi karibu zimeibuka hoja ya wananchi wengi ambao wamehoji namna ya kuwachagua wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza kwa shule za bweni.Hoja za wananchi zinaonesha wazi kuwa kila mzazi anatamani  mtoto wake achaguliwe katika shule za bweni. Akitoa ufafanuzi wa hoja za wazazi na walezu, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI

Na Barnabas Kisengi-Kongwa


SIKU za hivi karibu zimeibuka hoja ya wananchi wengi ambao wamehoji namna ya kuwachagua wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza kwa shule za bweni.Hoja za wananchi zinaonesha wazi kuwa kila mzazi anatamani  mtoto wake achaguliwe katika shule za bweni.


Akitoa ufafanuzi wa hoja za wazazi na walezu, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI anayesimamia Elimu, Dkt. Charles Msonde  amesema kuna vigezo wazi ambavyo vibatunika kuchagua wanafunzi hao.
Dkt. Msonde ametoa ufafanuzi huo wakati wa ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ya  kukagua ujenzi wa miundombinu ya madarasa yatakayopokea wanafunzi wa kidato cha kwanza,2023.


Amesema kuwa wanafunzi waliofaulu na kuwa na sifa ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  mwaka 2023 ni 1,073,941 na kati ya hao waliochaguliwa kujiunga na shule za bweni ni 4,224  ambao ni sawa na asilimia 0.39 ya wanafunzi wote waliochaguliwa.


Akifafanua ni kwa nini idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kwa shule za bweni ni ndogo, Dk Msonde alisema ni kutokana na ufinyu wa shule za bweni,Alisema kuwa idadi ya shule za Sekondari za Serikali zinazochukua wanafunzi wa kidato cha kwanza ni 4,307 na kati ya hizo shule za kutwa ni 4,269 na za bweni ni 38 tu ambazo zinauwezo wa kuchukua wanafunzi 4,224.
“Kutokana na idadi ndogo ya shule za bweni tulizonazo na ili watoto waweze kukaa darasani vizuri, kulala bwenini kwa mujibu wa muongozo, shule hizo 38 zina uwezo wa kupokea wanafunzi 4,224 ambao ni sawa na asilinia 0.39 tu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.”


Akizungumzia namna ya kuwapata wanafunzi kujiunga na shule za bweni, uchaguzi wa wanafunzi hao umekuwa ukizingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ya kuzingatia viwango vya ufaulu.
“Wale wenye viwango vya juu sana ndio waliochaguliwa, lakini hata hivyo waliofaulu kwa viwango vya juu pia ni wengi, hivyo mfumo ulitumika kuchagua wale waliofauli zaidi ya wenzao.”
“Hapa tunasema waliochaguliwa kwenda bweni wamepata daraja la kwanza A, lakini ukiangalia waliopata daraja hilo wapo wanafunzi 50,475, hivyo hata kwenye daraja hili la kwanza ipo kanuni iliyotumika ya kugawa nafasi za wanafunzi waliofaulu vizuri.”


Amesema  kuwa, shule za bweni zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni  kundi la kwanza ni lile lenye ufaulu wa juu, kundi la pili ni shule za bweni za ufundi na kundi la tatu ni shule za bweni kawaida.


Dk Msonde alisema kwa upande wa shule zenye ufaulu wa juu ziko saba zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 932 ambao ndio waliopangiwa.
Pia, shule za bweni za ufundi ziko tisa zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,323 wakai shule za bweni za kawaida zimechukua wanafunzi 1,816 na bweni umiliki wa mkoa 153.
” Ikumbukwe kuwa shule hizi za bweni ni za Kitaifa, hivyo uchaguzi wa wanafunzi wa kwenda katika shule hizo pia unafanyika kitaifa kwa maana kuwa kila mkoa na halmashauri nchini lazima zitoe wanafunzi watakaokwenda kusoma katika shule hizo.”
“Hapa tunaona wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja kwanza (A) wako 50,475 na kati ya hao waliochaguliwa ni 4,224, hivyo kwenye shule za bweni zenye ufaulu wa juu tunatumia uwiano wa idadi wa watahiniwa katika Mkoa  mara Idadi ya nafasi zote kwa watahiniwa waliofaulu zaidi gawanya kwa jumla ya watahiniwa wote kitaifa hapo utapata  idadi ya nafasi za bweni kwa watahiniwa waliofaulu zaidi kwenye Mkoa.”


Dkt. Msonde aliongeza, “kanuni hiyo hiyo itatumika kwenye Mkoa kupata idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kwenda kwenye shule zenye ufaulu wa juu kutoka Mkoa husika.”
“Kanuni hii pia itatumika kupata wanafunzi waliochaguliwa kwenye shule za bweni za ufundi kutoka kwenye mikoa yote nchini.”
Kwa upande wa shule za bweni kawaida, Dkt. Msonde alisema kanuni yake ni uwiano wa watahiniwa wote wa Darasa la Saba katika shule za vijijini au mazingira magumu katika Halmashauri mara idadi ya nafasi zote za bweni kwa wavulana na wasichana wa vijijini au mazingira magumu Tanzania bara gawanya na idadi ya watahiniwa wote wa darasa la VII katika shule za vijijini/mazingira magumu hapo utapata nafasi kwa kila Halmashauri.
“Ikumbukwe kuwa nafasi hizi ni kwa wanafunzi wote waliosoma shule za Serikali na Binafsi katika Mkoa na Halmashauri husika.”


Dkt Msonde alisema kwa shule za kutwa wanafunzi  1,069,717  walichaguliwa kwenda kwenye shule hizo ambapo kila wanafunzi aliyefaulu na kukosa nafasi kwenye ushindani wa shule za Bweni alipangiwa kwenye shule ya sekondari ya kutwa  iliyokaribu na shule ya msingi aliyosomea.
“Sambamba na kanuni na muongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mfumo ndio uliotumika kufanya chaguzi hizo hii kupunguza changamoto za kibanaadamu ambazo zingeweza kuleta mgongano wa kimaslahi.”


Dkt. Msonde aliongeza kuwa: “kila mwanafunzi aliyechaguliwa kwenda shule ya bweni anakidhi vigezo vyote hata ukiingia kwenye mfumo utaona kuwa vigezo vyake ni vya juu kuliko wengine waliokwenda kwenye shule za kutwa katika hili  watoto wa Taifa hili kutoka pembe zote za nchi wenye vigezo wamechaguliwa kwenda kwenye shule za bweni ili kuleta utaifa na umoja kwa watoto wetu. Alisema daraja la  A analipoata mwanafunzi ni kati ya jumla ya alama 241 hadi 300.
“Niweke wazi kuwa ufaulu wa daraja la kwanza yaani A unaanzia kwenye maksi 241 hadi 300,, na wazazi au walezi wanaona daraja ambalo mtoto wake amepata lakini sisi tunaoingia kwenye mfumo tunaona alama  sasa mtaona kwamba takribani wanafunzi  46,251 wenye ufaulu wa daraja la kwanza (A) wamepengiwa kwenye shule za kutwa kutokana na uhaba wa nafasi za bweni.
“Lakini wale waliopangiwa bweni wanaufaulu wa daraja la kwanza wa alama za juu zaidi kuliko wale 46,251 na ndio maana tulivyofika ukomo wa idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kwenda bweni wale waliobakia wenye ufaulu wa daraja la kwanza wote waliopangiwa kwenye shule za kutwa.”


Aidha, Dkt. Msonde alitumia fursa hiyo kuwasihi wazazi kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza, 2023 wanaripoti shule kwa wakati ili waweze kuanza masomo kwa awamu moja.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »