KASI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA WIZARA YA MAJI MJI WA SERIKALI YAMRIDHISHA AWESO

KASI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA WIZARA YA MAJI MJI WA SERIKALI YAMRIDHISHA AWESO

Na Barnabas Kisengi Mtumba-Dodoma Waziri wa Maji Jumaa Aweso  amefanya ziara maalumu ya Kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara ya Maji lililopo katika Eneo la Mtumba Mkoani Dodoma Linalogharimu Zaidi ya Tsh Billioni 22.9. Katika Ziara hiyo Waziri ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Barnabas Kisengi Mtumba-Dodoma


Waziri wa Maji Jumaa Aweso  amefanya ziara maalumu ya Kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara ya Maji lililopo katika Eneo la Mtumba Mkoani Dodoma Linalogharimu Zaidi ya Tsh Billioni 22.9.


Katika Ziara hiyo Waziri ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza zoezi la ujenzi wa majengo ya ofisi za Wizara zote na hususani Ofisi ya Wizara ya Maji yenye Jengo lenye uwezo wa kuhudumia  zaidi ya watu 518 na hivyo kuleta ufanisi kwa watumishi  katika utendaji wao wa kazi.


Aidha Waziri amempongeza Mkandarasi anayejenga mradi huo kwa kufanya kazi nzuri na kwa kasi na muda sahihi ambapo mpaka Sasa mradi umefikia asilimia 82 huku zikibaki asilimia 18 tu ili mradi huo uweze kukamilika.


Huu ni mwendelezo wa desturi alioanza nayo Waziri Aweso katika kuusimamia na kuufuatilia mradi huu tangu hatua za mwanzo kabisa hadi sasa akiwa na malengo ya kuona unakamilika kwa wakati na kwa viwango ambapo amekua akitembelea kujionea hatua za ujenzi mara kwa mara na amekiri hatua hii iliofikiwa imekidhi matarajio na matamanio yake.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »