Wajumbe wa Halmashauri kuu Taifa (NEC) Mwanza wataka CCM ijibu hoja kwa Usitarabu Majukwaani

Wajumbe wa Halmashauri kuu Taifa (NEC) Mwanza wataka CCM ijibu hoja kwa Usitarabu Majukwaani

Na Mwandishi Wetu Mwanza WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa wa mkoani Mwanza wamewaomba viongozi wenzao kujibu hoja majukwaani kwa hekima na busara wakizingatia utekelezaji unaofanywa na serikali yao. Kauli hiyo imetolewa  Jijini Mwanza na wajumbe hao, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na Elen Bogohe katika

Na Mwandishi Wetu Mwanza


WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa wa mkoani Mwanza wamewaomba viongozi wenzao kujibu hoja majukwaani kwa hekima na busara wakizingatia utekelezaji unaofanywa na serikali yao.


Kauli hiyo imetolewa  Jijini Mwanza na wajumbe hao, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na Elen Bogohe katika sherehe za kuwapokea baada ya kuchaguliwa katika vikao vikuu vya chama hicho vilivyokamilika hivi karibuni Jijini Dodoma.


Mabula amesema anamshukuru Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kufikiwa kwa maridhiano na vyama vingine vya kisiasa hapa nchini ili kuwezesha ushiriki wao katika mikutano ya hadhara.
Amesema kwa vile serikali ya awamu ya sita imeendeleza kazi zilizofanywa na awamu zingine za uongozi wa taifa hili hivyo haoni ni kwa nini CCM ishindwe kujibu hoja zitakazoibuliwa na vyama vingine kwa usitarabu.
“Ni jukumu letu kama viongozi wa chama kusimamia serikali yetu kutekeleza yale yote yaliyo katika ilani ya chama ili tupate maendeleo na hapo tutakuwa tunajibu hoja kwa vitendo” amesema Mabula.


Mabula amesema miradi mikakati katika mkoa wa Mwanza kama ujenzi wa soko la Kisasa jijini hapo, ujenzi wa kituo cha magari Nyegezi, ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza na daraja kubwa la Kigongo Busisi imeleta mapinduzi makubwa hapa nchini.  


Naye mjumbe wa NEC ya CCM Bogohe amesema kuwa baada kumalizika kwa chaguzi ndani ya chama wanalojukumu la kuhakikisha kuwa wanasimamia utekelezaji wa miradi yote iweze kukamilika kwa wakati na hapo watakuwa katika nafasi kubwa ya kujibu hoja toka kwa vyama vingine.
“Ujenzi wa vyumba vya madarasa ndani mkoa wetu ni kielelezo kikubwa kuwa serikali ya awamu ya sita inatekeleza kwa juhudi kubwa kazi za kuwaleteawatanzania maendeleo” alisema Bogohe.


Amewataka wanachama wa chama hicho kutobabaika bali wajibu hoja zitakazotolewa kwa busara kwani kuendelea kukamilishwa kwa miradi hiyo ni hatua nzuri kwao kujinadi bila hofu majukwaani.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »