BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA YATAKIWA KUSIMAMIA SHIRIKA HILO KUWA KITOVU CHA BIASHARA MTANDAO

BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA YATAKIWA KUSIMAMIA SHIRIKA HILO KUWA KITOVU CHA BIASHARA MTANDAO

Na Barnabas Kisengi Dodoma Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mhandisi Kundo Mathew ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta Tanzania kuifanikisha mpango mkakati wa Serikali wa kulifanya Shirika hilo kuwa kitovu cha Biashara Mtandao kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC).  Mhandisi

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mhandisi Kundo Mathew ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta Tanzania kuifanikisha mpango mkakati wa Serikali wa kulifanya Shirika hilo kuwa kitovu cha Biashara Mtandao kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC). 

Mhandisi kundo Ametoa agizo hilo Januari, 13,2023 wakati alipokuwa akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Nape Nnauye jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mhandisi Kundo ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha huduma na biashara zote za Posta zinatolewa kwa wananchi kupitia mfumo wa Posta Kiganjani unaowezesha wananchi kupata huduma zote za Posta kupitia kifaa chochote cha TEHAMA lengo ni kuwarahisishia wananchi kupata huduma za Posta popote walipo hususani kupitia Mfumo wa Anwani zao za makazi utakaowezesha kufikiwa mpaka mahali walipo.

Aidha, Naibu Waziri ameisistiza Bodi hiyo kuhakikisha ndani ya kipindi chao cha Uongozi wanatekeleza kikamilifu mikakati ya Serikali iliyowekwa ndani ya Shirika ikiwemo uanzishwaji wa wa vituo vya kutolea huduma za Serikali mahali Pamoja (one stop centres) kupitia ofisi za Posta kote nchini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Serikali kwa wananchi.


Katika hatua nyingine, Mhandisi Kundo ameongeza kuwa, Posta ni mojawapo ya Taasisi za Umma zilizopewa jukumu la kutoa huduma kwa wananchi hivyo kuitaka iongeze kasi katika kupanua matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa watumiaji hao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo ameahidi kutendea kazi majukumu yote waliyokabidhiwa na Serikali kwa manufaa ya Shirika na Taifa kwa ujumla. Naye Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo ametumia nafasi hiyo kumshkuru Mgeni Rasmi kwa kuweza kufika na kuzindua Bodi hiyo ya Shirika na kuahidi kushirikiana nayo kikamilifu kwa maslahi mapana ya Shirika.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »