MFUKO WA UWEKEZAJI WA ‘FAIDA FUND’ KULETA NEEMA KWA WANANCHI WA HALI ZOTE

MFUKO WA UWEKEZAJI WA ‘FAIDA FUND’ KULETA NEEMA KWA WANANCHI WA HALI ZOTE

Na Mwandishi Dar es salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Jenista Mhagama amesema mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa FAIDA FUND umeanzishwa kwa lengo la kuwanufaisha watanzania wote wa kipato cha chini, kati na cha juu ambao wamekuwa wakikabiliana na changamoto ya kupata mtaji wa kuwekeza

Na Mwandishi Dar es salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Jenista Mhagama amesema mfuko wa uwekezaji wa pamoja wa FAIDA FUND umeanzishwa kwa lengo la kuwanufaisha watanzania wote wa kipato cha chini, kati na cha juu ambao wamekuwa wakikabiliana na changamoto ya kupata mtaji wa kuwekeza kwenye masoko ya fedha na mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi. 


Waziri Mhagama amesema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  kuzindua Mfuko wa Faida (FAIDA FUND) unaoratibiwa na Watumishi Housing Investments (WHI).


Mhagama amesema kuwa, Mfuko wa Faida unatarajia kutoa gawio kubwa litakalokuwa na tija kwa wote ambao watawekeza kwenye Mfuko wa Faida kwa lengo la kujikwamua kiuchumi, hivyo elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili wajitokeze kwa wingi kununua vipande katika mfuko huo.
 “Mfuko wa Faida ni salama  kwa wawekezaji ambao wanataka kuepuka upotevu wa fedha, hivyo natoa wito kwa wanawake, vijana, wazee  na makundi mengine maalum kujitokeza  kununua vipande ili wanufaike na uwekezaji katika mfuko huu,” Alisisitiza Jenista Mhagama.


Sanjari na hilo, waziri Mhagama ametoa wito kwa watumishi wa umma, wanachama wa mifuko ya hifadhi za jamii na watanzania wote kujitokeza na kuwekeza katika Mfuko wa Faida ili wapate kipato kitakachoboresha shughuli zao za kiuchumi na maisha yao kwa ujumla.


Akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Jenista Mhagama kuzindua Mfuko wa Faida kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Naibu waziri Deogratius Ndejembi amempongeza Katibu Mkuu-UTUMISHI Dkt. Laurean Ndumbaro kwa kuisimamia vema WHI kujenga mfumo rafiki uliowawezesha wananchi kuwekeza kwenye mfuko huo ambao hivi sasa kiasi cha shilingi bilioni 13.5 kimewekezwa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ametoa wito kwa watumishi wa umma kuwekeza kwenye Mfuko wa Faida

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »