RUVUMA: WAZIRI BASHE AAMURU MBOLEA KUUZWA HADI SAA 12 JIONI

RUVUMA: WAZIRI BASHE AAMURU MBOLEA KUUZWA HADI SAA 12 JIONI

Na Barnabas Kisengi Ruvuma. Waziri wa Kilimo, Husein Bashe amemuomba Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Julius Ningu kuwawezesha wasambazaji wa mbolea kufanya kazi mpaka saa 12 jioni ili waweze kuwahudumia wakulima wanaohitaji huduma hiyo kwa msimu huu wa kilimo. Tuwawezesha kupata askari watakaolinda eneo la biashara na baadaye kuwasindikiza bank ili waweze kuweka pesa

Na Barnabas Kisengi Ruvuma.


Waziri wa Kilimo, Husein Bashe amemuomba Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Julius Ningu kuwawezesha wasambazaji wa mbolea kufanya kazi mpaka saa 12 jioni ili waweze kuwahudumia wakulima wanaohitaji huduma hiyo kwa msimu huu wa kilimo.


Tuwawezesha kupata askari watakaolinda eneo la biashara na baadaye kuwasindikiza bank ili waweze kuweka pesa za mauzo zikiwa katika hali ya uhakika na salama.
“Nawaagiza muendelee kuuza mbolea mpaka siku za jumamosi na  Jumapili and after working hrs tuongee na askari ili wawepo kuanzia saa 10 na saa 12 wawasindikize bank ili wakaweke pesa za mauzo,” Alisisitiza Waziri Bashe.


Waziri Bashe ametoa agizo hilo  Januari, 15, 2023 wakati wa ziara  katika ghala la mbolea la kampuni la  ETG  ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili mkoani Ruvuma.
Aidha, Waziri Bashe alimuagiza meneja wa ETG mkoani humo kufungua vituo vya uuzaji wa mbolea katika maeneo manne ndani ya Wilaya ya Songea ikiwa ni eneo la Mpitimbi, Peramiho, Mgazini na Magagula.


Akitoa maelekezo ya Serikali waziri Bashe amemtaka meneja huyo kuwasiliana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TRFA) ili  kuvisajili vituo hivyo na kuagiza kuwa vifanye biashara kama tawi la kituo cha biashara ETG Songea  ( extension ya Songea).
Kwa upande wake Meneja wa ETG Songea Vishnu Vardhan alikiri kupokea maelekezo ya waziri Bashe na kueleza kuwa kufuatia kuwepo kwa uhakika wa usalama wa fedha ya biashara, wapo tayari kuuza mpaka saa 12 jioni.
“Kama utasaidia bank sisi tutaendelea mpaka saa 12 jioni” Vishnu aliongeza. 


Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya mbolea la Premium, Angelina Haule akitoa uzoefu wake katika utekelezaji wa mpango wa mbolea za ruzuku amesema kufuatia taratibu za kununua mbolea za ruzuku ulivyo, wakulima wanaona wamebanwa na wanapitia hatua ndefu mpaka kupata  huduma ikiwa ni pamoja na kumtaka mkulima aliyesajiliwa kwenda mwenyewe kununua mbolea hiyo. 
Ameeleza kuwa, kutokana na malalamiko ya wakulima kampuni yake imeendelea kunawatia moyo na kuwataka wavumilie ili kuepusha udanganyifu kufuatia kiasi kikubwa cha fedha kilichotolewa na serikali ili kugharamia ruzuku ya mbolea.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »