NAIBU WAZIRI DUGANGE AMPA SIKU SABA MKURUGENZI TARIME KUKAMILISHA MAANDALIZI KUWAPOKEA WANAFUNZI 80

NAIBU WAZIRI DUGANGE AMPA SIKU SABA MKURUGENZI TARIME KUKAMILISHA MAANDALIZI KUWAPOKEA WANAFUNZI 80

OR TAMISEMI, TARIME Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime kukamilisha maandalizi ya kupokea wanafunzi 80 wa kidato cha kwanza waliopangiwa katika Shule mpya ya Sekondari Bukira ili wapokelewe na kuanza masomo.Ametoa maelekezo hayo Januari 16, 2023 wakati akikagua ujenzi wa

OR TAMISEMI, TARIME


Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime kukamilisha maandalizi ya kupokea wanafunzi 80 wa kidato cha kwanza waliopangiwa katika Shule mpya ya Sekondari Bukira ili wapokelewe na kuanza masomo.
Ametoa maelekezo hayo Januari 16, 2023 wakati akikagua ujenzi wa mpya ya Shule mpya ya Sekondari Bukira katika halmashauri ya Wilaya Tarime iliyotakiwa kukamilika na kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 9, 2023.

IMG-20230116-WA0162

Amesema ujenzi wa sekondari Bukira ulitakiwa kukamilika tarehe 30/06/ 2022 na kuanza kupokea wanafunzi mwaka huu lakini kutoka na changamoto za ukosefu wa usimamizi madhubuti imepekekea wanafunzi waliopangiwa katika shule hiyo kuanza masomo katika shule jirani ya Sirari.
Dkt. Dugange amesema Serikali ilitoa shilingi milioni 470 kujenga shule mpya ili kupunguza wingi wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Sirari pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya Ufundishaji na Ujifunzaji kwa wanafunzi.

IMG-20230116-WA0160

Aidha, Dkt. Dugange ameagiza Jengo la ICT na Jengo Maabara 3 yakamilike kabla ya tarehe 28 Februari 2023 ili kuwawezesha wanafunzi waliopangiwa kuanza shule kuyatumia kupata elimu kwa vitendo.
Shule Mpya ya Bukira ilitakiwa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza tarehe 9 Januari 2023 kutoka na changamoto cha Ukamilishaji wa baadhi Majengo imesababisba wanafunzi kuendelea na masomo katika Shule jirani ya Sirari hivyo watahamia katika Shule hiyo tarehe 23 Januari 2023 kutoka na Maelekezo yakiyotolewa

IMG-20230116-WA0157
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »