SOPHIA MJEMA AWATAKA VIONGOZI CCM KUCHANGAMSHA AKILI

SOPHIA MJEMA AWATAKA VIONGOZI CCM KUCHANGAMSHA AKILI

Na Mwandishi Wetu Dar es salaam Katibu mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amewataka watumishi wa Chama na maafisa wa idara yake ya Itikadi na Uenezi kuchangamsha akili na weledi katika kutekeleza majukumu yao. Mjema ambaye aliteuliwa January 14 2023  kupitia vikao

Na Mwandishi Wetu Dar es salaam


Katibu mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amewataka watumishi wa Chama na maafisa wa idara yake ya Itikadi na Uenezi kuchangamsha akili na weledi katika kutekeleza majukumu yao.

Mjema ambaye aliteuliwa January 14 2023  kupitia vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa vilivyofanyika January 14 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


Mjema amesema hayo wakati  akizungumza na Watumishi na maafisa hao, baada ya kufika kwa mara ya kwanza ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa bidii, umoja, ubunifu na kuhakikisha wakati wote wanakuwa mfano bora katika kuendelea kujenga, kutunza na kulinda haiba nzuri ya Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wake Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mjema ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo mpya awali alikuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, amesisitiza kazi kubwa iliyopo mbele ya watumishi hao ni kuendelea kuyasemea kwa wananchi mazuri yanayofanyika ili wayafahamu.

Aidha Mjeme amewataka Viongozi kueleza uzuri wa CCM, kusikiliza kero au changamoto walizo nazo Wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuendelea kuwajengea uwezo wanachama na viongozi kupitia mafunzo.

“Kazi zote hizi hazipaswi kusubiri, tuanze sasa na tuendelee mbele”, Amesisitiza Mjema .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »