SERIKALI YAANZA KUCHUKUA HATUA KWA SHULE ZINAZOFUNDISHA WANAFUNZI MAADILI MABAYA

SERIKALI YAANZA KUCHUKUA HATUA KWA SHULE ZINAZOFUNDISHA WANAFUNZI MAADILI MABAYA

Na Barnabas Kisengi Dodoma Serikali kupitia wizara ya Elimu imeanza kuchukua hatua kufuatia ripoti iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari juu ya uwepo wa baadhi ya shule zinayofundisha wanafunzi maadili mabaya, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma. Prof.Mkenda amesema kuwa Wizara ya

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Serikali kupitia wizara ya Elimu imeanza kuchukua hatua kufuatia ripoti iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari juu ya uwepo wa baadhi ya shule zinayofundisha wanafunzi maadili mabaya, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.


Prof.Mkenda amesema kuwa Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia  tayari Imeshamwaagiza Kamishina wa Elimu Tanzania, Mzibiti Ubora wa Shule Nchini na Mwanasheria wa Wizara ya Elimu  wameanza uchunguzi katika hizo shule zilizotajwa na baada ya hapo watakuja na majibu.
“Hatuwezi kusema kesho au keshokutwa watupatie majibu maana ni suala linalohitaji uchunguza na kupatikane majibu ya usahihi ili tuepuke kuharakisha mambo alafu baadae mambo yakaharibika ndio maana tumemwagiza Kamishina aa elimu mwenyewe sio Mwakilishi na Mwanasheria wa Wizara na sio Mwakilishi tupate majibu yaliyokamilika,”Amesisitiza Prof.Mkenda 

Waziri Mkenda amesema kuwa wizara imekusudia kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa namba maalumu kwaajili ya kutoa taarifa ya vitendo hivyo katika shule za umma au binafsi hapa Nchini
“Katibu Mkuu atatoa namba maalum kwa ajili ya kila mmoja kupiga simu pale ambapo atabaini kuna vitendo hivyo vichafu shuleni,”amesema Prof.Mkenda 
Aidha Prof.Mkenda amesema kuwa Serikali itahakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kwani vitaondoa uaminifu kwa wazazi juu ya kuwapeleka watoto wao shule.


Prof.Mkenda amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itashirikiana na Wizara zingine za kisekta kupata ufumbuzi na kukomesha matukio kama hayo yanayotokea mashuleni.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »