OFISA YA BUNGE YAANZISHA MABONANZA KWA AJILI YA WABUNGE

OFISA YA BUNGE YAANZISHA MABONANZA KWA AJILI YA WABUNGE

Na Barnabas Kisengi Dodoma Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Aksoni amesema Ofisi ya Bunge imeanzisha utaratibu wa kuwa na Bonanza la michezo kwa waheshimiwa wabunge na watumishi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt Tulia amesema mabonanza hayo yatafanyika mara nne kila mwaka katika vipindi vya mikutano

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Aksoni amesema Ofisi ya Bunge imeanzisha utaratibu wa kuwa na Bonanza la michezo kwa waheshimiwa wabunge na watumishi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Dkt Tulia amesema mabonanza hayo yatafanyika mara nne kila mwaka katika vipindi vya mikutano ya Bunge ambapo kutakuwa na mabonanza matatu madogo katika mikutano mifupi ya Bunge na Bonanza moja kubwa wakati wa Mkutano wa Bajeti.


Aidha Spika wa Bunge amesema leongo la mabonanza hayo ni kutoa fursa ya kufaamiana na kutambuana kwa waheshimiwa wabunge, watumishi wa Bunge pamoja na wadau mbalimbali katika Mazingira nje ya Ofisi ya Bunge kwa lengo la kufaamiana zaidi na kujenga umoja utakaosaidia kuleta Utekelezaji wa majukumu yetu ya kibunge.


Dkt Tulia amesema kuwa Bonanza la kwanza litafanyika siku ya Jumamosi January 28 2023 Katika viwanja vya shule ya sekondari ya John Merlin ambapo Bonanza hilo litaanza na matembezi yatakayoanzia katika chuo cha Mipango Dodoma na kuishia katika viwanja vya shule ya sekondari ya John Merlin.
“Bonanza hilo litahusisha michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa Pete, mpira wa kukapo, mpira wa wavy,mpira wa meza, Pool table, kurusha mishare, riadha ya kutembea kwa haraka, mchezo wa bao, draft, karata, kuvuta Jamba, kurusha tufe, kufukuza kuku,kukimbia kwa magunia, kukimbia na glass ikiwa na maji, kukimbia na kijiko, kushindana kunywa soda na kushindana kula chakula” amesema Spika Dkt Tulia.


Aidha Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Aksoni amesema baada ya Bonanza hilo kumalizika anatarajia waheshimiwa wabunge na watumishi wa Bunge watakuwa wamejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza kupunguza hatari ya kupata maradhi sugu yasiyo ambukiza kama vile kisukari, shindikizo la damu, uzito ulio pitiliza, kuondosha dalili za msongo wa mawazo na kuimarisha Afya ya akili.


Dkt Tulia Aksoni amesema kuwa kuanzishwa kwa Bunge Bonanza hakufuti ushiriki Wetu katika michezo mingine ya kirafiki inayohusiana na michezo ya mabunge mengine ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kauli mbiu yetu isemayo. “Bunge Bonanza Shiriki Michezo, Jenga Taifa lenye Afya”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »