MARIAM DITOPILE AHAIDI MIFUKO 100 ZA SARUJI UJENZI WA BWENI SHULE YA VIZIWI KONGWA

MARIAM DITOPILE AHAIDI MIFUKO 100 ZA SARUJI UJENZI WA BWENI SHULE YA VIZIWI KONGWA

Na Barnabas Kisengi Dodoma MBUNGE wa Viti Maalum Mariam Ditopile ameahidi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule maalum Kongwa kitengo cha viziwi ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu. Msaada huo umefuatia baada ya kusomwa kwa taarifa ya shule inayoonyesha uwepo wa wanafunzi wanaoshindwa kuhudhuria masomo


Na Barnabas Kisengi Dodoma


MBUNGE wa Viti Maalum Mariam Ditopile ameahidi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule maalum Kongwa kitengo cha viziwi ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.


Msaada huo umefuatia baada ya kusomwa kwa taarifa ya shule inayoonyesha uwepo wa wanafunzi wanaoshindwa kuhudhuria masomo kutokana na umbali mrefu na wakati mwingine kupata tishio la fisi wakiwa njiani.


Akizungumza Januari 28,2023,kwenye ziara yake shuleni hapo akiwa katika maadhimisho ya kuelekea miaka 46 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mariam amesema kupitia changamoto alizozisikia ameguswa kuanzisha ujenzi wa bweni ili kuwasaidia watoto hao.

IMG-20230127-WA0204

“Changamoto zenu za uhaba wa walimu,bweni nimezisikia,wakati nafanya mpango wa kufuatilia serikalini utatuzi wa hizi changamoto ni vyema na sisi tuanze,kwa kuanzia natoa mifuko ya saruji 100,”amesema.


Amewataka umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Dodoma kukaa na kuweka mikakati ya kushiriki ujenzi huo iwe kwa michango kutoka kwa viongozi wote wa umoja huo mkoa na nguvu kazi pia.
“Uongozi mzuri ni ule unaoacha alama,hebu viongozi shirikianeni mchangishane hata 2,000 kila mmoja,tuna nguvu kazi ya kutosha kupitia vijana,njooni hapa siku moja tuanze kazi ya kuchimba msingi,tuanze ujenzi,ili hata serikali ikija kusaidia ikute tumeshaanza,”Amesisitiza Ditopile

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »