RC SENYAMULE AWATAKA WANAUME KUACHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

RC SENYAMULE AWATAKA WANAUME KUACHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Na Moreen Rojas,Dodoma. Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa vijana wa kiume na wanaume pamoja na wale wote wanaotekeleza vitendo vya kikatili dhidi watoto na wanawake kuacha mara moja kwani kundi kubwa linaloathirika na vitendo hivyo ni watoto na wanawake. Senyamule ametoa wito huo January 28, 2023 katika hospitali ya Rufaa

Na Moreen Rojas,Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa vijana wa kiume na wanaume pamoja na wale wote wanaotekeleza vitendo vya kikatili dhidi watoto na wanawake kuacha mara moja kwani kundi kubwa linaloathirika na vitendo hivyo ni watoto na wanawake.

Senyamule ametoa wito huo January 28, 2023 katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma .(General Hospital) alipokua Akizindua kituo jumuishi cha utoaji wa huduma kwa manusura wa vitendo vya Ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto na Wanawake huku akisema Dodoma Ni mkoa ambao ukatili wa kijinsia Unatendeka na ukatili dhidi ya watoto na Wanawake.

“Mradi huu wa USAID AFYA YANGU umekuja wakati muafaka hapa Jijini na tunashukuru kwamaana mkoa huu pia una Changamoto ya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto na Wanawake japo pia hata watoto wa kiume nao wanaathirika na vitendo hivyo vya kikatili katika maeneo mengi ya Mkoa Wetu.”. Alisema Senyamule

Manusura wa magonjwa ya kikatili wamekua wakipata Changamoto katika kupata huduma kwa haraka nakwa uratibu kutokana na mtawanyiko wa maeneo ya huduma muhimu wanayohitaji ikiwemo huduma za afya,ustawi wa jamii na huduma za Kisheria.

kutokana na Changamoto hiyo Senyamule amesema jengo hilo la kutoa huduma jumuishi kwa manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ni moja ya malengo ya mpango jumuishi wa utoaji huduma kwa walengwa iliyozinduliwa mwaka 2013 kwa lengo la kuhakikisha huduma inatolewa kwa manusura wa ukatili kwa haraka, uratibu mzuri, na kurahisisha mfumo wa rufaa kwa manusura kwa kupata huduma maalum kama Masada wa Kisheria.

“Hali hii imesababisha baadhi ya manusura kukosa huduma kwa wakati na kupata madhara yakiwemo maambukizi ya virusi vya Ukimwi, Ulenavu wa kudumu,Mimba Zisizotarajiwa na mimba za utotoni zaidi kutokana na vitendo vya ukatili Walivyofanyiwa”amesema Senyemule

“Aidha baadhi ya manusura kurubuniwa kupotea kwa ushahidi ambao ungesaidia manusura kupata haki yake pindi shauri linapofikishwa katika vyombo vya Sheria,kutumia garama kubwa katika kufikia maeneo ya kupatia huduma hivyo kusababisha matukio mengi ya ukatili, kutokutolewa taarifa katika vyombo vya Sheria hali Iliyosababisha manusura kukosa huduma mbalimbali pamoja na haki za kisheria”.amesema Senyamule

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema uwepo wa kituo hicho jumuishi katika mkoa wa utawawezesha manusura wa vitendo vya ukatili kupata huduma kwa haraka ili kuwawezesha kupata haki zao katika vyombo vya Sheria.

Senyamule Amewaagiza wahudumu wa jengo ambao wanatoa huduma kwa manusura kufanya kazi masaa 24 kwani vitendo vya kikatili vinatokea muda wowote hivyo kuanzisha utaratibu wa kuwa katika hospitali hiyo muda wote na kuwaasa kutumia vifaa kwa umakini mkubwa na kwaweledi mkubwa kwa manufaa ya kuchakata takwimu za manusura wanaopatiwa huduma katika jengo hilo lililozinduliwa ndani ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Chip Lyons Rais wa shirika la EGPAF ambao ni wadau Waliofadhili ukarabati wa jengo hilo la utoaji wa huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili amesema mradi huo unatakribani miaka 13 tangu kuanzishwa mwaka 2003 kutokana na ushirikiano mzuri na Viongozi wa Tanzania hata uongozi wa mkoa wa Dodoma.

Naye Anna Hoffman Nibu Mkurugenzi wa Shirika la afya la USAID amesema mradi huo Unatekelezwa kwa mikoa ya Dodoma, Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Tabora huku Ukilenga kufikia maeneo mengi hapa Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »