WAZIRI MKUU AWASISITIZA WABUNGE WASHIRIKI MICHEZO

WAZIRI MKUU AWASISITIZA WABUNGE WASHIRIKI MICHEZO

Na Barnabas Kisengi Dodoma Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Januari 28, 2023 ameshiriki Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi na sekondari ya John Merlin ya jijini Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wabunge na wananchi wengine washiriki katika michezo ili kuipa miili yao nguvu na uwezo wa

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Januari 28, 2023 ameshiriki Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi na sekondari ya John Merlin ya jijini Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wabunge na wananchi wengine washiriki katika michezo ili kuipa miili yao nguvu na uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

“Michezo kwetu sisi wabunge ni muhimu zaidi kwa sababu inatufanya tuwe na afya bora zaidi na pia michezo inasaidia watu kukutana pamoja na kuimarisha undugu, kujenga urafiki pamoja na kukuza vipaji. Nampongeza Mhe Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwa ubunifu huu wa kuanzisha Bunge Bonanza ambalo litakuwa linafanyika mara kwa mara.”amesema waziri Mkuu

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na wabunge, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Watumishi wa Bunge pamoja na maafisa wengine wa Serikali walio shiriki katika Bunge Bonanza lililohudhuriwa na wabunge jijini Dodoma

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia amesema Bunge Bonanza litakuwa linafanyika mara nne kwa mwaka lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi umuhimu wa kushiriki katika kufanya mazoezi ili jamii iweze kuwa na afya bora zaidi na kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza kama kisukari,shindikizo la damu na kuondokana na msongo wa mawazo.

” Hii fursa kwetu sisi wabunge ni nzuri licha ya kujiwekea miili yetu vizuri pia tunajenga afya ya mwili na kuepukana na maradhi mbalimbali pia inatupa fursa ya kuwa karibu na watumishi wa Bunge na wananchi kwa ujumla na kujenga Mahusiano ya karibu na wenzetu katika majukumu ya utendaji kazi wetu ndani ya Bunge na nje ya Bunge na Amesema Bunge Bonanza linguine linatarajia kufanyika June 24 mwaka huu”Amesema Dkt Tulia

Naye, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Katibu wa Michezo wa Baraza hilo Mhe Nassor Salim Ali (Jazeera) ambaye amemuwakilisha Spika wa Baraza la Wawakilishi amesema baraza litaendelea kushirikiana na Bunge ili kudumisha undugu kupitia michezo pamoja na shughuli mbalimbali wanazozifanya.

“Tunamshukuru RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kudumisha Muungano wetu ambao umeleta amani na utulivu hadi Sasa”amesema Mhe Nassor Salim Ali

Awali, Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Mhe Festo Sanga amesema pamoja na mambo mengine bonanza hilo limeanzishwa ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ambaye amekuwa akiihamasisha jamii kushiriki katika kufanya mazoezi kwa ajili ya kuupa mwili afya na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.

Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni timu ya Bunge na ya watumishi wa Bunge ambapo timu ya Bunge ilipata kombe la mshindi wa jumla baada ya kuishinda timu ya Watumishi wa Bunge katika michezo mingi.

Michezo iliyochezwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa meza, mpira wa mikono, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kunywa soda, kuvuta kamba, kurusha tufe na mashindano ya kula wali maharagwe.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »