DODOMA: WAKUU WA WILAYA WATAKIWA KUZINGATIA VIAPO VYAO

DODOMA: WAKUU WA WILAYA WATAKIWA KUZINGATIA VIAPO VYAO

Na Moreen Rojas, Dodoma. Katibu  Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Bi. Jasmini Awadhi amewataka wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa kuheshimu na kuviishi viapo vyao walivyoviapa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.  Bi Awadhi ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa kiapo cha 

Na Moreen Rojas, Dodoma.


Katibu  Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Bi. Jasmini Awadhi amewataka wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa kuheshimu na kuviishi viapo vyao walivyoviapa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. 


Bi Awadhi ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa kiapo cha  Ahadi ya Uadilifu kwa Mkuu wa wilaya ya Chemba Mh Gelard  Mongela  katika hafla fupi iliyofanyika  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma January  30, 2023.
“hakikisheni mnajitoa kutumikia viapo mlivyotoa mbele yetu na kuviweka katika kumbu kumbu zenu za kila siku ili viwasidie kuyakunbuka yale yote yaliyoelezwa katika viapo hivyo mnapotekeleza majukumu yenu ya kila siku”.


Aidha Bi Awadhi amempongeza Mkuu wa wilaya ya Chemba  kwa kuteuliwa kwake na amesema kuwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekupa heshima kubwa ya kuiongoza wilaya ya Chemba.


Katibu huyo Msaidizi aliwapongeza wakuu wengine wa wilaya waliahamishiwa kikazi Katika Mkoa wa Dodoma katika wilaya ya Bahi Mhe Godwini Gondwe na Wilaya ya Mpwapwa Mhe Sophia Kizig.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amewataka wakuu wa Wilaya Zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanajipanga kutumikia Wananchi kwa namna ya kimakao Makuu huku akiwataka kuhakikisha changamoto ya Elimu kwa Mkoa wa huu inakwishwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi mashuleni.
“Suala la utoro mashuleni kuhakikisha linakwisha hakikisheni watoto wote wanaostahili kwenda darasa la kwanza na kidato cha kwanza hawaachwi nyuma na kufuatilia kila mwanafunzi kwa undani na mzazi yoyote atakaye kwamisha suala la elimu kushughulika naye ipasavyo kwa kufuata taratibu na sheria za nchi”Alisisitiza Senyamule.


Mkuu wa Mkoa amewahimiza wakuu wa wilaya za Dodoma kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia  suala la utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuikijanisha Dodoma pamoja na kuzingatia na kuhimiza wananchi kupanda miti walau minne kwa kila kaya.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »