Timu za Usimamizi Shirikishi kutoka Tamisemi imetoa Wito kwa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Ruvuma

Timu za Usimamizi Shirikishi kutoka Tamisemi imetoa Wito kwa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Ruvuma

Na Mwandishi Wetu Ruvuma Timu ya Usimamizi shirikishi   kutoka  Idara ya Afya kutoka Ofisi ya RAIS TAMISEMI  imetoa wito kwa timu za uendeshaji wa huduma za afya  Mkoa wa Ruvuma kuhahakisha inaimarisha na kusimamia utoaji wa  huduma bora  za afya katika vituo vya kutolea huduma. Wito huo umetolewa Januari, 31, 2023 na Mkurugenzi wa huduma

Na Mwandishi Wetu Ruvuma


Timu ya Usimamizi shirikishi   kutoka  Idara ya Afya kutoka Ofisi ya RAIS TAMISEMI  imetoa wito kwa timu za uendeshaji wa huduma za afya  Mkoa wa Ruvuma kuhahakisha inaimarisha na kusimamia utoaji wa  huduma bora  za afya katika vituo vya kutolea huduma.


Wito huo umetolewa Januari, 31, 2023 na Mkurugenzi wa huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe  Ofisi ya RAIS TAMISEMI Dkt.Ntuli Kapologwe  alipozungumza kwa niaba ya  timu ya usimamizi shirikishi  kutoka TAMISEMI katika kikao kazi kati ya timu hiyo na   timu ya uendeshaji wa huduma za afya  Mkoa wa Ruvuma.
Amesema kuwa jukumu pekee la watoa huduma za afya  nchini ni kuhakikisha  vituo vya kutolea huduma za afya nchini vinahudumia wananchi  saa 24  na  kutoa huduma bora za afya  ili kwenda sambamba na nia ya Serikali ya kusogeza huduma hiyo katika jamii.


Dkt Kapologwe ameitaka timu hiyo kuhakikisha inasimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya akisisitiza kuwa mapato hayo yatumike katika kuboresha utoaji wa huduma ya afya ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma.


Pamoja na kikao hiko timu hiyo ilitembelea na kukagua utoaji wa huduma za afya pamoja na utekelezaji wa  ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya   katika Vituo vya Afya  Lilambo, Masigira pamoja na Mletele vilvyopo katika Manispaa  ya Songea.


Timu  imemshauri  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea  kuhakikisha kuwa huduma ya mama na mtoto inaanza kutolewa katika kituo cha afya Lilambo kuanzia tarehe 25 Februari, 2023.


Aidha timu hiyo imetoa wito kwa Waganga Wakuu wa Halmashauri Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha Vituo vyote vya kutolea huduma za afya  vinatoa  huduma ya chanjo katika maeneo ambayo yapo  mbali na vituo vya afya ( huduma za  mkoba) ili kuwapunguzia wananchi adha na gharama ya kufuata huduma hiyo vituoni hapo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »