MAAFISA UGANI WATAKIWA KUSHUKA KWA WAKULIMA

MAAFISA UGANI WATAKIWA KUSHUKA KWA WAKULIMA

Na Barnabas Kisengi Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule  amefanya kikao na Maafisa ugani kutoka Wilaya za halmashauri zote za mkoa wa Dodoma ikiwa ni jitihada za kuleta mapinduzi ya uchumi unaotokana na sekta ya Kilimo Mkoani Dodoma.Senyamule amesikitishwa na takwimu za matumizi ya ardhi ya kilimo inayotumiwa na wakulima ukilinganisha na ukubwa

Na Barnabas Kisengi Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule  amefanya kikao na Maafisa ugani kutoka Wilaya za halmashauri zote za mkoa wa Dodoma ikiwa ni jitihada za kuleta mapinduzi ya uchumi unaotokana na sekta ya Kilimo Mkoani Dodoma.
Senyamule amesikitishwa na takwimu za matumizi ya ardhi ya kilimo inayotumiwa na wakulima ukilinganisha na ukubwa wake na mazao wanayopata katika kipindi cha mavuno.
“Uchumi wetu wa Mkoa unategemea kilimo,lakini ni kweli kwamba takwimu zetu ziko chini sana na ile historia ya Dodoma kuwa maskini ni kama inaendelea kuishi.Tunataka historia ibaki kusimuliwa na siyo kuendelea kuishi Tunataka kilimo kiwe chenye tija,na serikali imeendelea kuiboresha sekta hii Kwa vifaa,pembejeo , wataalamu wa kilimo kuanzia ngazi ya Mkoa, wilaya,kata,mitaa hadi vijijini”amesema Senyamule.


“Kama ardhi tunayo ,watu wapo na wataalam wapo Sasa ni wapi tunakwama kukifanya kilimo chetu kiwe cha tija Katika Mahitaji ya msingi ya mwanadamu ,Chakula ni miongoni mwa hitaji la muhimu sana”Amesisitiza Senyamule
Tunataka Kufanya Mapinduzi makubwa ya kilimo,na Kwa kuanzia tayari ujenzi wa Mabwawa mapya umeanza katika halmashauri zetu.Tuko tayari kuiunga Mkono kauli ya Mhe.Rais ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu Cha Chakula barani Afrika.Mabadiliko haya katika sekta ya Kilimo yanawategemea sana ninyi wataalam wetu na leo tutaazimia mwelekeo mpya wa kuyatafuta mapinduzi katika sekta hiyo ya kilimo katika Mkoa wetu.


Aidha Mkuu wa Mkoa amemuagiza katibu tawala wa Mkoa Kufanya ukaguzi wa agizo la Kila Afisa ugani kuwaona shamba darasa katika eneo lake. “Wanasema ni rahisi zaidi watu Kufanya unachofanya kuliko unachosema na pia nyinyi maafisa sasa sio muda wa kukaa Ofisini nendene mkawatembelee wakulima mashambani. 
“Kila afisa ugani akitimiza wajibu wake na kuacha kufanya kazi kwa mazoeya na tabia ya kukaa Ofisini au kuzunguka zunguka kwenye jengo la halmashauri huu sio muda wenu nendeni kuwatembelea maafisa ugani huko kwenye kata na vijiji muone wanawasaidiaje wakulima hapo mtakuwa mmetimiza wajibu wenu kama wakuu wa idara na ukiona huwezi kufanya hivyo tupishe mapema kabla hatujakufikia maana hapa Makatibu tawala wote wa Wilaya watakuwa wanawafuatilia na kutoa ripoti Juu ya utendaji wenu wa kazi hasa katika Kipindi hichi cha kilimo”Amesisitiza Senyamule.


Mbali na Wataalam hao,kikao hicho pia kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Dodoma,Makatibu tawala wa Wilaya,Meya wa Jiji,Wenyeviti wa halmashauri zote za Mkoa na Wakuu wa idara na wawakilishi wakazi wa Mpango wa Chakula Duniani WFP

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »