AJALI YAUA 17 TANGA WAKIENDA KUZIKA MOSHI (+VIDEO)

AJALI YAUA 17 TANGA WAKIENDA KUZIKA MOSHI (+VIDEO)

Watu 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 4, 2023 wilayani Korogwe mkoani Tanga.Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba leo imeeleza kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na Majeruhi 12. Ajali hiyo imetokea

Watu 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 4, 2023 wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba leo imeeleza kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na Majeruhi 12.

Screenshot_20230204-100931


Ajali hiyo imetokea usiku katika eneo la Magira Gereza Kata ya Magira Gereza Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, barabara ya Segera – Buiko.
“Ajali hii imesababisha vifo 17 na majeruhi 12 ambao majina yao wote hayajafahamika, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo na majeruhi wawili wamebaki Hospitali ya Korogwe kwa matibabu.
“Ajali hii imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi” imeeleza taarifa hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametumia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter kutoa salama za Pole kwa wahanga wa ajali hiyo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »