SERIKALI WA AWAMU YA SITA YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA AFYA YA MAMA NA MTOTO

SERIKALI WA AWAMU YA SITA YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Na Mwandishi Wetu Mikese. CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesisitiza moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na RAIS Dkt SAMIA SULUH HASSAN ni kuhakikisha huduma za afya hasa ya Mama na Mtoto inaendelea kuboreshwa ili Wananchi wapate huduma zilizo bora zinazoambatana na vifaa tiba vya kisasa. Kauli hiyo imetolewa na na Katibu wa

Na Mwandishi Wetu Mikese.


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesisitiza moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na RAIS Dkt SAMIA SULUH HASSAN ni kuhakikisha huduma za afya hasa ya Mama na Mtoto inaendelea kuboreshwa ili Wananchi wapate huduma zilizo bora zinazoambatana na vifaa tiba vya kisasa.


Kauli hiyo imetolewa na na Katibu wa Halimashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Itikadi na Uenezi CCM Taifa Bi Sophia Mjema alipokuwa Akizungumza na  wananchi wa Mikese Mkoani Morogoro baada ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amesema lengo mojawapo la Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha Wana boresha huduma za afya kwa kutoa huduma bora na vifaa tiba vilivyobora.


“Katika Kituo cha Afya Mikese tumeona jengo la Mama na Mtoto lakini tumeona vifaa tiba ambavyo ni bora na vya kisasa kabisa kikiwemo kitanda cha kujifungulia akina mama mnajua ukishapata uchungu unakaa unahangaika hangaika lakini kitanda chenyewe kinakwambia geuka kulia, geuka kushoto  kwa hiyo wanawake wanajifungua kwa raha Sasa bila shida”Amesema Mjema
“Yote hayo yanafanyika kwa sababu ya RAIS SAMIA SULUH HASSAN anahakikisha anasimamia na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM  lakini kwa namna ambavyo  Serikali imeamua kuboresha huduma za mama na mtoto baada ya mama kujifungua anakwenda kwenye eneo maalum kwa ajili ya kuangalia afya zao kama ziko vizuri lakini hata akienda nyumbani bado kuna utaratibu wa kufuatilia ili kujua maendeleo. Yote hayo yanafanyika chini ya Chama Cha Mapinduzi kwa kutekeleza ilani yetu”amesema Mjema.


Aidha Mjema amesema Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona mama anajifungua vizuri na aendelee kukuwa akiwa na akili zake vizuri huku akitumia nafasi hiyo kukumbusha wazazi kuzingatia siku 1000 katika kumlea mtoto ikiwa pamoja na kunyonyweshwa vizuri na kulishwa vizuri na kupata virutubisho.
“Mtoto akitoka hapo hao ndio wanakuwa ma-genius(vipaji) wa baadae kwa hiyo akina baba , akina mama tuhakikishe tunasomesha watoto wetu lakini tunahakikisha tunamsomesha mtoto wa kike vizuri zaidi kwani mtoto wa kike ana kumbuka nyumbani kwa hiyo haya yote yanayofanyika katika huduma za afya ni kwa ajili ya kuhakikisha tunamsaidia mama anayeleta binadamu mwingine kwenye dunia hii”Alisisitiza Mjema.


Lakini katika kuhakikisha binadamu huyo anakuwa vizuri ni jambo la kuweka mikakati kwamba binadamu huyu anayezaliwa Tanzania azaliwe vizuri, alelewe vizuri kwenye zile sikue 1000 zake na apate lishe nzuri baada ya hapo atakapokuwa ndipo tutakuwa na watu wenye akili watakaotoka hapa Tanzania.
“Ili tufike huko lazima kuwepo na mikakati ikiwemo ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto RAIS Dkt SAMIA SULUH HASSAN ni Mama hivyo ameona mbali na amekuja na mikakati ya kuona mbali na anajua akikutayarisha hivi Sasa baadae nchi itakuwa inaongoza Afrika lakini duniani , tunataka tukimbie twende katika nchi ambazo zimeendelea zaidi,”amesema Mjema.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »