”Serikali inaratibu utolewaji wa elimu na huduma za afya kwa watoto mashuleni”Naibu Waziri Dkt. Festo.

”Serikali inaratibu utolewaji wa elimu na huduma za afya kwa watoto mashuleni”Naibu Waziri Dkt. Festo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) amesema Serikali kupitia Halmashauri imeendelea kuratibu utolewaji wa elimu na huduma za afya kwa watoto walioko shuleni, hususani kwenye magonjwa ya Malaria, minyoo, kichocho, saratani ya mlango ya kizazi, afya ya kinywa na meno pamoja na macho. Amesema hayo leo tarehe 06 Februali 2023

May be an image of 1 person and indoor
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) amesema Serikali kupitia Halmashauri imeendelea kuratibu utolewaji wa elimu na huduma za afya kwa watoto walioko shuleni, hususani kwenye magonjwa ya Malaria, minyoo, kichocho, saratani ya mlango ya kizazi, afya ya kinywa na meno pamoja na macho.

Amesema hayo leo tarehe 06 Februali 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Asha Abdullah Juma akiyetaka kujua Je, kuna mpango gani wa kushughulikia huduma za Afya kwa uchunguzi tiba na kujikinga katika Shule za Msingi na Sekondari.

Dkt. Dugange amesema huduma ya Afya kinga na tiba shuleni ni afua muhimu inayotekelezwa na Serikali kuwajengea watoto uelewa wa kujikinga na magonjwa, huduma hiyo inahusisha utoaji wa elimu ya afya, utambuzi wa magonjwa katika hatua ya awali pamoja na uratibu wa kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Amesema Katika kipindi cha mwaka 2021/22, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya iligawa vyandarua 3,104,401 kwenye shule za Msingi 7,639 kwa uwiano wa chandarua kimoja kwa kila mtoto, chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi ilitolewa kwa wasichana 623,501 dozi ya kwanza na 472,460 dozi ya pili.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Vita Rashid Kawawa alitaka kujua Je, ni lini Serikali itatoa fedha Shilingi milioni 100 kumalizia Kituo cha Afya Mchomoro zilizoahidiwa na Rais wa Awamu ya Tano?.

Akijibu Swali hilo, Dkt. Dugange amesema Kituo cha Afya Mchomoro kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kimejengwa kwa nguvu za Wananchi, fedha za Halmashauri, Mfuko wa Jimbo, pamoja na wadau, Ujenzi wake ulianza mwaka 2019, na kiasi cha Shilingi milioni 52.5 zimetumika kujenga jengo la wagonjwa wa nje ambalo limekamilika na linatumika.

Amesema kwa kuwa kituo hicho hakina miundombinu muhimu ya kukiwezesha kutoa huduma za ngazi ya kituo cha afya, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/24, itatenga shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »