*MAAJABU YA TAI*

*MAAJABU YA TAI*

Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu,yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu. Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake magumu na makali yanakosa uwezo wa kunyakua chakula, mdomo wake uliochongoka unapinda, mabawa yake yanakuwa mazito na kunata kwenye kifua chake hivyo kumfanya kuwa


Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu,yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu.

Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake magumu na makali yanakosa uwezo wa kunyakua chakula, mdomo wake uliochongoka unapinda, mabawa yake yanakuwa mazito na kunata kwenye kifua chake hivyo kumfanya kuwa mzito kuruka na kuwa mwenye kasi ndogo.

Katika hali hiyo ndege huyo hubakiwa na maamuzi mawili; aidha akubali kufa au afanye mabadiliko katika mwili wake ili aendelee kuishi miaka 30 iliyobakia.

Akichagua kufanya mabadiliko kwenye mwili wake humchukua siku 150 sawa na miezi 5, hivyo huenda katika kilele cha mlima mrefu na kujificha katika pango ambapo watu na wanyama wengine wanaoweza kumzuru hawafiki. Ndipo huanza kujivua kucha, midomo na mbawa zake zilizozeeka huku akisikilizia maumivu makali, baada ya mabadiliko hayo hurudi katika hali yake ya mwanzo ya kuweza kuruka kwa kasi na kupata chakula chake kizuri (fresh meat).

Bado siku chache sasa ili tumalize mwaka, hivyo lazima ufanye mabadiliko makubwa sana katika maisha yako, ujivue baadhi ya tabia ambazo zimeleta Ukakasi katika maendeleo yako ya 2020 japo zingine ni ngumu kuziacha na pengine zitakusababishia Maumivu lakini “no pain no gain” lazima ujivue baadhi ya Marafiki wasiolekea unakoelekea, jivue Uvivu, jivue Uongo, jivue Mahusiano yasiyo na Amani, jivue Ulevi, jivue kulala sana, jivue Uasherati, jivue kuahirisha ahirisha Mipango yako, na mengine yanayofanana na hayo.

Ikiwa Tai anafanya maamuzi ya kubadilika akiwa na miaka 40, hata wewe bado hujachelewa…Fanya mabadiliko sasa, ingia Mwaka 2021 ukiwa na Tabia mpya na Mtazamo Mpya kwa ajili ya kuanza safari yako mpya ya maisha.


 *MUNGU Akubariki Sana katika Maamuzi yaliyo sahihi.”*

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »