WANANCHI WA NKASI KUNUFAIKA NA HEKTA 10 TOKA HIFADHI YA LOASI

WANANCHI WA NKASI KUNUFAIKA NA  HEKTA 10 TOKA HIFADHI YA LOASI

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wanatarajiwa kumegewa eneo lenye ukubwa wa hekta 10,828 kutoka  katika Msitu wa Hifadhi wa Loasi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na makazi. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema hayo bungeni kwa Niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu


Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wanatarajiwa kumegewa eneo lenye ukubwa wa hekta 10,828 kutoka  katika Msitu wa Hifadhi wa Loasi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na makazi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amesema hayo bungeni kwa Niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe.Aida Khenani kuhusu mkakati wa Serikali wa kuwapatia wananchi maeneo ya kulima kutoka kwenye mapori na hifadhi ambazo hazina wanyamapori.


Naibu waziri Amesema kufuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta, Wilaya ya Nkasi inapaswa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kukidhi mahitaji ya wananchi kwa kuwa wilaya hiyo haina uhaba wa maeneo bali inakabiliwa na changamoto ya mgawanyo na mtawanyiko wa makazi na shughuli za kibinadamu.


Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhe. Mary Masanja amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi na kujichukulia sheria mkononi kwa kuwadhuru wahifadhi wanaolinda rasilimali za Taifa.
 “Tunasikitishwa sana na vitendo vya wananchi wanaojichukulia sheria mkononi na kudhuru askari wetu wa uhifadhi. Askari hawa wanalinda rasilimali hizo kwa niaba ya Watanzania, tunaomba wananchi washiriki kuyalinda maeneo haya wasijichukulie sheria mkononi” Amesisitiza Mhe. Masanja.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »