SIMBA AFA KIMOJA UGENINI

SIMBA AFA KIMOJA UGENINI

KLABU ya Simba imeshindwa kutamba katika mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya AC ya nchini Guinea. Horoya AC ilianza kupata bao kupitia kwa nyota wao kutoka nchini Senegal, Pape Ndiaye aliefunga kwa kichwa dakika ya 18 kipindi cha

KLABU ya Simba imeshindwa kutamba katika mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya AC ya nchini Guinea.

Horoya AC ilianza kupata bao kupitia kwa nyota wao kutoka nchini Senegal, Pape Ndiaye aliefunga kwa kichwa dakika ya 18 kipindi cha kwanza.

Katika mchezo huo licha ya kipindi cha kwanza Horoya AC kutawala mchezo, kipindi cha pili Simba walirudia na hali ya kutaka kurudisha bao na kuweza kupata ushindi kwenye mchezo huo lakini matumaini yakayeyuka baada ya Nahodha wao John Bocco kukosa nafasi nyingi za wazi.

Kwenye mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Lansana Conte General nchini Guinea, Aishi Manula  alionesha umwamba wake kwa kuchomoa penati ambayo ilisababishwa na Josh Onyanga kuushika mpira ndani ya boksi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »