Na Barnabas Kisengi-Arusha Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Deogratius Ndejembi ameipongeza baadhi ya taasisi za umma, ukiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuweza kuwafikia wananchi kwa kutumia matumizi ya TEHAMA. Naibu waziri Ndejembi amesema hayo jijini Arusha katika ufunguzi sherehe za
Na Barnabas Kisengi-Arusha


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Deogratius Ndejembi ameipongeza baadhi ya taasisi za umma, ukiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuweza kuwafikia wananchi kwa kutumia matumizi ya TEHAMA.
Naibu waziri Ndejembi amesema hayo jijini Arusha katika ufunguzi sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao kinachokutanisha wataalam wa TEHAMA kutoka serikalini
“Leo nimejionea kwenye mabanda pale PSSSF wameweza kuweka App ili kuweza kuona michango inavyokwenda Hivyo nielekeze e-GA kuendelea kufanya tafiti ili kuleta bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta za viwanda, biashara na uwekezaji kulipeleka mbele taifa letu kimaendeleo”amesema Naibu Waziri Ndejembi.
Naibu Waziri Ndejembi Amesema katika hili nitoe pongezi pia kwa taasisi ambazo tayari zimeweza kuwafikia wananchi kiurahisi Zaidi na kuondoa urasimu wa makaratasi.
Aidha Naibu Waziri Ndejembi amezishauri taasisi nyingine za umma kuitumia TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za serikali kwa haraka.
Huduma za PSSSF Kiganjani na PSSSF Mtandaon. Huduma hizi ni suluhisho kwa wanachama, wastaafu na waajiri kuweza kupata huduma popote walipo na muda wowote kwa kutumia simu janja au kompyuta bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za PSSSF.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *