MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA SONGWE

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA SONGWE

Na Mwandishi Wetu Songwe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Februari 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la hospitali ya wilaya ya Songwe.Ujenzi wa hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya

Na Mwandishi Wetu Songwe


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Februari 13, 2023 ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la hospitali ya wilaya ya Songwe.
Ujenzi wa hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ambapo Halmashauri inatarajia kukamilisha Mradi huu machi, 31,2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo tayari vifaa vyake vimepokelewa.


Ujenzi katika hospitali hiyo inahusisha Ujenzi wa Majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, Mionzi, Maabara, ufuaji, Famasia, Utawala na Jengo la Mama na Mtoto, Ujenzi wa Wodi tatu za Magonjwa Mchanganyiko.
Majengo mengine ni jengo la Huduma ya dharula na Nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la Upasuaji, jengo la Uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za Upasuaji (Wanaume na Wanawake)

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »