Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kutumia Shilingi 575,000,000 kupeleka Vifaa vya Tehama kwa Shule 16 za Sekondari

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kutumia Shilingi 575,000,000  kupeleka Vifaa vya Tehama kwa Shule 16 za Sekondari

Na Morin Rojas Dodoma Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema kuwa mfuko huo unatarajia kutumia shilingi 575,000,000 ,kwa ajili ya Mradi wa Kupeleka Vifaa Maalum vya TEHAMA vya Kujifunzia kwa Shule 16 Zenye watoto wenye mahitaji maalum hapa nchini.Bi Mashiba ameyasema hayo  Februari 13,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea utekelezaji

Na Morin Rojas Dodoma


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema kuwa mfuko huo unatarajia kutumia shilingi 575,000,000 ,kwa ajili ya Mradi wa Kupeleka Vifaa Maalum vya TEHAMA vya Kujifunzia kwa Shule 16 Zenye watoto wenye mahitaji maalum hapa nchini.
Bi Mashiba ameyasema hayo  Februari 13,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo mbele ya waandishi wa habari.

Aidha Bi Mashiba Amezitaja Shule hizo zitakazonufaika ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Mpwapwa (Dodoma), Sekondari ya Mkolani (Mwanza), Sekondari ya Kashaulili (Mpanda-Katavi), Sekondari ya Morogoro (Morogoro), Sekondari ya Shinyanga (Kishapu-Shinyanga), Sekondari ya Wavulana Songea (Songea), Sekondari ya Kazima (Tabora) na Sekondari ya Haile Selassie (Mjini Magharibi).


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSFA) Amesema vifaa vitakavyopelekwa katika shule hizo ni pamoja na na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu).
“Shule hizi 16 zitanufaika  naamini vifaa hivi vitakapowafikia hawa watoto wenye mahitaji maalum vitawasaidia katika kujifunza na kufikia malengo na nia ya mfuko wa UCSAF ni kuhakikisha nchi nzima inaunganishwa na mawasiliano,”amesisitiza Mashiba

Kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, Shule 150 zitafikishiwa vifaa vya TEHAMA,Bajeti yake ikiwa ni  1,950,000,000/- na vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi kusoma katika shule hizo 811,”amesema Mashiba
Akizungumzia hali ya Mawasiliano nchini Mashiba amesema kuwa Mwaka 2009 Population Coverage ya Huduma za Simu ilikuwa asilimia 45 (45%) wakati kwa sasa imeongezeka hadi kufikia asilimia 96 (96%),Teknolojia ya 2G coverage yake ni 96%,3G ni 72%,4G ni 55% na Geographical Coverage ya 2G ni 69%; 3G ni 55% na 4G ni 36%.


Kwa upande wa Ujenzi wa Minara Vijijini Mtendaji huyo amesema UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654, Wakazi 15,130,250 ambapo Minara 1,087 yenye vijiji 3,378 na wakazi 13,320,750 na Utekelezaji unaendelea katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 kwa ruzuku iliyotolewa yaTZS bilioni 199 ikiwemo pia Mradi wa kimkakati wa Zanzibar, Minara 42, Shehia 38 ruzuku TZS bilioni 6.9.
Bi Mashina amesema kuwa Jumla ya shule 811 zimefikishiwa Vifaa vya Tehama ambapo kwa wastani kila shule imepewa Kompyuta 5, Printa 1 na Projekta 1.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »