TCRA YAANDAA KIKAO KAZI CHA SIKU MBILI KUADHIMISHA SIKU YA REDIO DUNIANI

TCRA YAANDAA KIKAO KAZI CHA SIKU MBILI KUADHIMISHA SIKU YA REDIO DUNIANI

Na Barnabas Kisengi Dodoma Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeandaa kikao kazi cha siku mbili cha kuadhimisha siku ya Redio Duniani na kuongozwa na kauli mbiu inayosema “Mchango wa Sekta ya Utangazaji katika kukuza uchumi wa kidijitali” ikimaanisha sekta ya utangazaji inafanya kazi kwa njia za kisasa za kimtandao zaidi ambapo njia hii inasaidia kuchangia pato

Na Barnabas Kisengi Dodoma

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeandaa kikao kazi cha siku mbili cha kuadhimisha siku ya Redio Duniani na kuongozwa na kauli mbiu inayosema “Mchango wa Sekta ya Utangazaji katika kukuza uchumi wa kidijitali” ikimaanisha sekta ya utangazaji inafanya kazi kwa njia za kisasa za kimtandao zaidi ambapo njia hii inasaidia kuchangia pato la taifa kwa kasi.

Akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, Naibu Waziri Mhe. Kundo Mathew amesema Serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya habari ili iwe na tija kwa jamii ya Watanzania.

“Mambo mengi yamefanyika kwa kipindi kifupi kwenye sekta ya mawasiliano nchini katika Serikali hii ya awamu ya Sita kama vile kujenga ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi. Hongera kwa siku ya Redio duniani inayotokana na mkutano wa 36 wa UNESCO ambapo hapa nchini tuanza kuadhimisha mwaka 2012. Natoa rai kwa vyombo vya utangazaji kuzingatia kauli mbiu ya “Redio na amani”, tuhakikishe matangazo ya Redio yanafika pembezoni ili kila mmoja apate haki ya kupata matangazo. Miaka ya 90 tuliweza kuhama kutoka njia za analojia kwenda dijiti na Serikali imeshuhudia changamoto za kiuchumi za vyombo vya utangazaji hivyo imepunguza ada za usajili na urushaji wa matangazo ili kuhakikisha utangazaji unaleta tija”

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye naye amekua miongoni mwa wageni waalikwa kwenye ufunguzi wa Mkutano huo, ameishukuru sekta ya habari nchini kwani inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali jambo ambalo linasaidia kupiga maendeleo kwa haraka.

“Dodoma tuna radio 10 zilizosajiliwa kutoa huduma kwani ni haki kwa vyombo vya habari kupata habari kutoka Serikalini na tumekua tukitekeleza hilo kupitia vyombo hivyo. Tunaamini vyombo vya Dodoma vitalenga zaidi katika kukuza uchumi wa kidijitali. Serikali inashirikiana vizuri na vyombo vya habari na tunavishukuru sana” Ameongeza Mhe. Senyamule

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasilino Nchini TCRA, Bw. Jabir Kuwe Bakari, amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi kidijiti kwa kuwa matangazo mengi yamehamia kwenye njia hiyo na pia ameelezea dhumuni hasa la Mkutano wa mwaka huu;

“Nchini Tanzania tuna watoa huduma za habari wapatao 787, mkutano huu umeandaliwa kwa lengo la kutafakari mchango wa sekta ya utangazaji katika jamii kwani vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuchangia kukuza uchumi wa kidijiti nchini. Mkutano huu utajadili changamoto zinazoikabili sekta ya utangazaji pamoja na hali ya sasa ya sekta hii na kutoa maazimio. Pia Mkutano huu umekwenda sambamba na maandalizi ya maonyesho ya vifaa mbalimbali vya utangazaji yatakayofanyika hapa” Amesema Bw. Bakari

Sekta ya utangazaji nchini imefanya Mkutano wake wa mwaka wa watoa huduma ya utangazaji nchini ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye aliyewakilishwa na Naibu Waziri wake Mhe. Kundo Andrea Methew. Mkutano huo kwa mwaka huu umefanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete ukishirikisha wadau wote wa sekta ya utangazaji nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »