Wanawake Nchini wameaswa Kuwania Fursa ya Kuchukuwa Mikopo kwa Malengo

Wanawake Nchini wameaswa Kuwania Fursa ya Kuchukuwa Mikopo kwa Malengo

Na Moreen Rojas Dodoma Katibu Mtendaji wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bi.Beng’i Issa amewaasa wanawake kuchukua mikopo kwa malengo na sikufanya shughuli ambazo zitawakwamisha kurejesha mikopo hiyo.Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC). Aidha amesema kuwa

Na Moreen Rojas Dodoma


Katibu Mtendaji wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bi.Beng’i Issa amewaasa wanawake kuchukua mikopo kwa malengo na sikufanya shughuli ambazo zitawakwamisha kurejesha mikopo hiyo.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).


Aidha amesema kuwa miradi yote inapita vijijji mbalimbali na lazima wawashirikishe wananchi wa eneo husika ili wanufaike na miradi hiyo kwani lengo ni kumfikia kila mwananchi ya hali ya chini na kuwainua kiuchumi.
Amesema baraza hilo limejita pia kuwawezesha vijana na wanawake kwani hao ndio watu wenye malengo na wanaorejesha mikopo kwa wakati na uaminifu mkubwa.
“Uwezeshaji wa wanawake hizi ni program zinazowasaidia wanawake kuwawezesha kiuchumi kwani ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha jamii nzima hivyo tumelenga kupeleka fedha kwenye makampuni ya wanawake na vikundi vya wanawake” amesema Bi Issa.


Aidha Bi Issa amesema kazi yao kama baraza ni kusukuma na kuonyesha hapa kuna tatizo kwa kushirikiana na serikali pamoja na kuwa na mazingira rafiki ya uwekezaji kwa mtanzania mwenyewe na mwekezaji wa nje.
“Tunasimamia mifuko ya uwezeshaji tunaita mifuko ya uwezeshaji kwa sababu tunatoa mikopo moja kwa moja kwa wananchi awe mkulima,mfugaji au mfanyabishara.


Aidha ametoa rai kwa wananchi hasa wanawake kuachana na mikopo isiyorasmi na ambayo haitambuliki na serikali(kausha damu) kwani lengo la mikopo hiyo ni kuwafilisi na kuwapotezea malengo badala yake ni kujiongezea mizigo na kushindwa kufikia n a kutimiza malengo waliyojiwekea na badala yake ni kufilisika kwa kutoa vitu vya thamani.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »