DC MWEMA AONGOZA KONGAMANO NA KIKAO CHA KWANZA CHA WADAU WA ELIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO

DC MWEMA AONGOZA KONGAMANO NA KIKAO CHA KWANZA CHA WADAU WA ELIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO

Na Mwandishi Wetu Chamwino Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remedius Mwema  ambaye pia Kwa sasa anakaimu wilaya ya Chamwino kufuatia mkuu wa wilaya hiyo kuwa likizo  februari 16.2023 ameongoza kikao Cha kwanza kati ya vikao viwili kwa mwaka cha wadau wa maendeleo ya  elimu katika halmashauri hiyo. Kikao hicho chenye lengo la kujadili maendeleo na

Na Mwandishi Wetu Chamwino


Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remedius Mwema  ambaye pia Kwa sasa anakaimu wilaya ya Chamwino kufuatia mkuu wa wilaya hiyo kuwa likizo  februari 16.2023 ameongoza kikao Cha kwanza kati ya vikao viwili kwa mwaka cha wadau wa maendeleo ya  elimu katika halmashauri hiyo.


Kikao hicho chenye lengo la kujadili maendeleo na changamoto ya elimu Kwa shule za msingi na sekondari,kikao ambacho  kimefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo Ma Afisa elimu,Ma Afisa tarafa,Walimu wakuu ,wakuu wa idara,Waratibu Elimu,Vyama vya siasa n.k.


Mkuu wa wilaya  Mwema amewataka wadau hao wa maendeleo ya elimu kukitumia kikao hicho kuijenga Chamwino yenye ufanisi katika sekta ya elimu Kwa kuyaeleza mafanikio na kuzijadili Changamoto zinazokwamisha maendeleo ya elimu katika halmashauri hiyo.
“Nimefurahi sana kualikwa kuhudhuria kikao hiki,ninaomba kikao hiki kitusaidie kuyabainisha maeneo yanayotukwamisha”
“Serikali chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kutuletea pesa za miradi ya maendeleo ya elimu zikiwemo za ujenzi wa miundo mbinu ya vyumba vya madarasa,madarasa,walimu n.k lakini ndugu zangu uwepo wa miundo mbinu hii hautakuwa na tija kama wanafunzi hawatapelekwa shule”
“Siku chache zilizopita nikiwa katika kufuatilia maendeleo ya elimu katika wilaya yetu ya Chamwino,nilibaini kuwa bado Kuna idadi ya wanafunzi hawajaripoti shuleni na Kati ya wanafunzi 10 wa 4 hawapo shule,wako mikoani wanafanya kazi za ndani,hili halikubaliki”


Aidha mkuu huyo wa wilaya ameeleza umuhimu wa chakula cha wanafunzi mashuleni na kama wilaya wamewekeza katika kilimo Kwa kuagiza mashamba yote ya shule yalimwe na kwamba baada ya mavuno watawaeleza wazazi na walezi umuhimu wa kuchangia chakula Kwa ajili ya wanafunzi.


Aidha nawaagiza Waheshimiwa madiwani  kuwajibu Kwa hoja wote wanaopotosha juu ya juhudi za serikali katika ujenzi wa miundo mbinu ya vyumba vya madarasa Kwa kusema , vyumba vimejengwa lakini wanafunzi wanakaa chini.Tufanye tathmini ya uwepo na upungufu wa madawati na tuweke mikakati ya kudumu katika swala zima la maendeleo ya wilaya yetu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »