Wanafunzi 323 wa kidato cha Kwanza wakiendelea na Masomo kwenye shule Mpya ya Nasa Matu,Kiteto.

Wanafunzi 323 wa kidato cha Kwanza wakiendelea na Masomo kwenye shule Mpya ya Nasa Matu,Kiteto.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ameshuhudia Wanafunzi zaidi ya 323 wa kidato cha Kwanza wakiendelea na Masomo kwa wakati mmoja katika vyumba vya madarasa saba kwenye shule Mpya ya Nasa Matui iliyopo wilaya Kiteto. Amejionea hali hiyo tarehe 22 Februari 2023 wakati alipofika Shuleni hapo kukagua ujenzi wa miundombinu

May be an image of 2 people, people standing and outdoors
May be an image of 16 people, people sitting and people standing
May be an image of 9 people, people sitting and people standing

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ameshuhudia Wanafunzi zaidi ya 323 wa kidato cha Kwanza wakiendelea na Masomo kwa wakati mmoja katika vyumba vya madarasa saba kwenye shule Mpya ya Nasa Matui iliyopo wilaya Kiteto.

Amejionea hali hiyo tarehe 22 Februari 2023 wakati alipofika Shuleni hapo kukagua ujenzi wa miundombinu ya Shule Mpya ya Nasa Matui iliyogharimu Milioni 470.

“Nimejionea Wanafunzi wa Kidato cha kwanza zaidi ya mia tatu katika awamu moja wakiendelea na masomo katika Madarasa saba kati ya nane yaliyojengwa katika Shue hii, na nimeelezwa kuwa hilo darasa moja lililosalia litajaa muda wowote” amesema Dkt. Dugange.

Dkt. Dugange amesema hali hiyo inaonesha muamko mkubwa wa elimu na kuthamini fedha za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alizotoa kuboresha utoaji wa elimu nchini kwa kujenga shule za kata zaidi ya 235 kwa wakati mmoja.

Aidha, Dkt. Dugange amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI inaenda kujipanga kwa kutenga fedha za kujenga madarasa mengine kwa ajili ya Wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka ujao wa 2024.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Kiteto, Mhe. Mbaraka Batenga amesema Wanafunzi waliopangiwa kuanza masomo katika Shule ya Nasa Matui ni 373 na walioripoti ni wanafunzi 332 sawa na asilimia 89 ya wanafunzi waliopagwa katika Shule hiyo.

Ofisi ya Rais, TAMISEMI kupitia Mradi wa kuboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ilitoa shilingi milioni 470 ya Ujenzi wa shule mpya ya Kata kwa kila Halmashauri kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa 8, jengo la utawala 1, maabara 3, maktaba 1, chumba cha TEHAMA 1, matundu ya vyoo 20 (wasichana 10 na wavulana 10), ununuzi wa tenki la maji 1, ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji na kunawa mikono.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »