Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewataka watendaji wa TARURA kila mmoja kwa nafasi yake atekeleze na kusimamia majukumu yake kwa weledi na ufanisi. Hayo ameyasema leo Februari 21, 2023 wakati alipokutana na kuzungumza na Mameneja TARURA Mkoa, Wilaya Wakuu wa Idara na Vitengo wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewataka watendaji wa TARURA kila mmoja kwa nafasi yake atekeleze na kusimamia majukumu yake kwa weledi na ufanisi.
Hayo ameyasema leo Februari 21, 2023 wakati alipokutana na kuzungumza na Mameneja TARURA Mkoa, Wilaya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini – TARURA kwa lengo la kufahamu changamoto za Taasisi hiyo lakini kujua majumukumu ya kazi zinazotekelezwa kwa kila Idara.
Amesema kila mmoja kwa nafasi yake ajue ni sehemu ya kutoa matokeo chanya kwa jamii ili kuendana na malengo ya Serilkali ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amesisitiza uwepo wa ushirikiano katika kazi bila kujali nafasi ya mtu na cheo alichonacho itasaidia umoja lakini pia ufanisi na uzalishaji bora wa kazi bila kujali aina ya kada za watu sababu wote ni watumishi na kila mmoja anahaki ya kutoa mchango wake kwa Taifa ili kufikia malengo ya Serikali.
Amewataka Viongozi hao kusimamia kazi za miradi yao kwa kufuata taratibu za kazi zilizopo lakini pia taratibu za Utumishi wa Umma.”simamieni utendaji wa kazi kila mtu katika eneo lake lakini ili kuwe na ufanisi na ubora wa kazi ushirikiano ni kitu muhimu”.
Niwatake msimamie maadili ya kazi na kuwa waaminifu na waadilifu na tuepuke “shortcut (njia za mkato)” katika kazi sababu “shortcut zinazokiuka maadili na utaratibu wa kazi mwisho wake hazina msaada ni vema kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria za kazi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Mhandisi Florian Kabaka ameishukuru Serikali na kusema Bodi hiyo itaendelea kuishauri TARURA kwa kufuata misingi ya kazi sababu inamchango mkubwa katika utoaji wa huduma amesema mpaka sasa imani ya wananchi kwa TARURA ni kubwa hivyo jukumu lao ni kuhakikisha taasisi hiyo inaendana na kasi ya Serikali hasa katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara na pia maadili ya Utumishi wa Umma.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *