”Wanganga Wakuu hamasisheni wananchi kujiunga na Mfuko wa CHF”.Waziri Kairuki.

”Wanganga Wakuu hamasisheni wananchi kujiunga na Mfuko wa CHF”.Waziri Kairuki.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewaelekeza Wanganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanatoa huduma bara za afya ili kuwahamasisha wananchi kuendelea kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya kwa Jamii(CHF). Kairuki ameyasema hayo leo Februari 22, 2023 jijini Dodoma wakati wa kuufunga mkutano

May be an image of 10 people, people sitting, people standing and text that says 'Mkutano Mkuu wa Mwaka wa SAUA NA SERIKALIZA MITAA Wakuu wa Mikoa na Halmashauri Waganga Kauli Mbiu Uboreshaji wa Huduma za Afya ni Nguzo ya Kufikia Afya kwa Wote Mhe. Ummy Mw Wazini WaznwA wa Februari 20-22, 2023 Ukumbi wa Mabeyo Bodoma EpiC Mhe. Angellah Kairuk (Mb) 60 Delaitha 5'
May be an image of 3 people and indoor
May be an image of 9 people, people standing and text that says 'wakuu wa Mikoa na Halmashauri waganga Kauli Mbiu Uboreshaji wa Huduma za Afya ni Nguzo ya Kufikia Afya kwa Wote mmy A Mwalimu (Mb) Afya Februari 20-22 2023 Ukumbi wa Mabeyo, Dodoma USAID Mhe.AngellahKairukiMb) Mhe. Angellah Kairuki wa Nchi OR TAMISEMI WIDH DPGR NSA'

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewaelekeza Wanganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanatoa huduma bara za afya ili kuwahamasisha wananchi kuendelea kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya kwa Jamii(CHF).

Kairuki ameyasema hayo leo Februari 22, 2023 jijini Dodoma wakati wa kuufunga mkutano mkuu wa mwaka wa Wanganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri.Amesema uelimishaji huo uendane sambamba na uboreshaji wa huduma kwa wateja, upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

Amesema pamoja na mafanikio ya yaliyopatikana kutokana na matumizi ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF) ambayo ni ongezeko la michango ya wanachama kutoka Sh bilioni 2.2 kwa mwaka 2018 hadi shilingi bilioni 30.2 kwa mwaka 2022, bado jamii inahitaji kuelimishwa kuhusu kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa jamii iliyoboreshwa.

Aidha, Kairuki amewaagiza waganga wakuu hao kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma zinazokusudiwa kwa wananchi.

Amesema uchambuzi wa utekelezaji wa miradi hiyo unaoneshajumla ya miradi 208 sawa na asilimia 14 ipo katika hatua ya chini ya lenta, miradi 106 sawa na asilimia 8 ipo katika hatua ya upauaji na miradi 845 sawa na asilimia 58 ipo katika hatua ya umaliziaji.

“Ninawaagiza miradi iliyopo kwenye upauaji ikamilike ifikapo tarehe Februari 28 mwaka huu na ile iliyopo kwenye lenta iikamilike kabla au ifikapo Machi 31 mwaka huu.

”Waziri Kairuki amesema moja ya kigezo kitakachotumika kupima utendaji kazi wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri ni ni utekelezaji wa majukumu yao kwa weledi na kuwataka kutimiza wajibu wao wa kutoa huduma bora kwa wananchi.Pia amewataka kuhakikisha wanashirikiana na idara nyingine pamoja na wakaguzi wa ndani kukagua bidhaa za afya na kitakuwa kiashiria cha ufanisi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »