Trilioni 4 kutatua changamoto ya umeme kukatika ovyo.

Trilioni 4 kutatua changamoto ya umeme kukatika ovyo.

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) linatarajia kutumia trilioni 4 kwa ajili ya kuweza kutatua changamoto ya umeme kukatika ovyo ikiwemo kununua transfoma imara,mita za umeme pamoja na ununuaji wa nguzo.Kaimu Mkulugenzi huduma kwa wateja Martin Mwambene Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika la umeme Tanzania

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) linatarajia kutumia trilioni 4 kwa ajili ya kuweza kutatua changamoto ya umeme kukatika ovyo ikiwemo kununua transfoma imara,mita za umeme pamoja na ununuaji wa nguzo.
Kaimu Mkulugenzi huduma kwa wateja Martin Mwambene Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO).
Mwambene amesema kuwa mradi wa umeme Rusumo kuanza kuingiza umeme kwenye gridi ambapo umefikia asilimia 80 na nchi zinazotarajia kunufaika ni pamoja na Tanzania,Rwanda na Burundi.
Aidha Mwambene Amesema kituo cha miito ya simu ndio namna bora ya kupata huduma tanesco kwa haraka zaidi kwani kituo kina watu ambao wana weledi mkubwa tofauti na hapo zamani ukitaka huduma mpaka uwe na ndugu yako anayefanya kazi tanesco na lengo la kituo hicho ni kuhakikisha ndani ya masaa 24 tunatatua matatizo ya watanzania nchi nzima.
“Tumeimarisha mifumo ya wateja kwa kuwa na huduma ya miito ya simu na nawahakikishia kwamba hakuna mtu anayepiga simu na kujibiwa vibaya na hata ukijibiwa vibaya tuna uwezo wa kuweza kujua ni nani amekujibu vibaya na hatua kali kuchukuliwa” Amesema Mwambene.
“Pia tunahuduma nyingine ya N_connect inayosaidia mteja kupata huduma zote akiwa nyumbani bila hata kufika ofisini na kuepuka wajanja wa mjini(vishoka) Amesisitiza Mwambene
Mwambene ameelezea kuwa  Miradi yote sio miradi ya siku mbili kwahiyo serikali yetu ianjitahidi kuhakikisha wanatatua changamoto ya umeme kwani ni kiu ya serikali kuhakikisha tunamaliza kabisa tatizo la umeme,njia ya kudumu iko katika kuimarisha gridi.
Aidha Amesema kuwa inapothibitika kwamba nyumba imeungua na tatizo ni tanesco,basi tanesco watawajibika kulipa fidia kwa muhusika ila ikiwa tatizo sio tanesco basi shirika halitawajibika na haliwezi kuhusika na kulipa fidia.
“Tanesco hatuuzi nguzo ila tunatoa huduma ya umeme,hivyo kwa wale ambao wanaunganisha umeme kwa wenzao ambao wana nguzo wanapaswa kulipia gharama kidogo na kufidia gharama za aliyenunua nguzo” Amesisitiza Mwambene.
Mwambene amesema mchakato wa smartmita unaendelea na mita hizo ni za gharama na majaribio yanaendelea kufanyika kwa baadhi ya mita ili kuweza kuona ni nani anaweza akatumia huduma hii kwa kukidhi vigezo.
Kwa upande wake Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi mkuu wa kitengo cha habari maelezo Ndg.Gerson Msigwa amewapongeza Tanesco kwa namna ambavyo inajitahidi kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuweza kuhakikisha hadi kufikia 2025 umeme uwe umewafikia watanzania wote hususani wa vijjini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »