Tume ya vyuo vikuu inaendelea kuimarisha mifumo ya uthibiti ubora.

Tume ya vyuo vikuu inaendelea kuimarisha mifumo ya uthibiti ubora.

Katibu Mtendaji wa tume ya vyuo vikuu nchini Prof.Charles Kihampa amesema kuwa tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na mifumo ya ndani ya vyuo vikuu ili kuhakikisha vyuo vikuu vinaendana na mwelekeo wa serikali.Prof.Kihampa amesema hayo  Februari 22,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa

Katibu Mtendaji wa tume ya vyuo vikuu nchini Prof.Charles Kihampa amesema kuwa tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na mifumo ya ndani ya vyuo vikuu ili kuhakikisha vyuo vikuu vinaendana na mwelekeo wa serikali.
Prof.Kihampa amesema hayo  Februari 22,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za tume ya vyuo vikuu Tanzania Kwa kipindi Cha miaka ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
Prof kihampa Amesema kuwa Tanzania imelenga kuwa Taifa la watu wenye maarifa,ujuzi,weledi na uwezo wa kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi Kwa manufaa ya wananchi wake ifikapo mwaka 2025 pamoja na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Aidha amesema tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi,wahadhiri na maofisa wa vyuo vikuu vya Umma na binafsi hapa nchini Kwa lengo la kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa taasisi zao.
Kuhusu kuongezeka Kwa fursa za masomo ya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu nchini,Prof.Kihampa amesema kuwa program za shahada ya kwanza zimeongezeka kutoka 157,770 mwaka 2020/2021 hadi 172,168 mwaka 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la nafasi 14,398 sawa na asilimia 9.1
Pia idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu imeongezeka kutoka 259,266 mwaka 2020/2021 hadi 295,919 mwaka 2021/2022 sawa na asilimia 14.1 idadi hii inatarajiwa kuongezeka Kwa mwaka wa masomo 2022/2023
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) ni taasisi ya Serikali, iliyoundwa mwaka 2005 Kwa Sheria ya vyuo vikuu sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »