Waziri Aweso,Mhandisi Sanga wameshiriki Mkutano wa Maswala ya Huduma ya Maji Duniani WWIS,London.

Waziri Aweso,Mhandisi Sanga wameshiriki Mkutano wa Maswala ya Huduma ya Maji Duniani WWIS,London.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga pamoja na ujumbe wa Wizara ya Maji wameshiriki Mkutano maalum unaohusiana na Maswala ya Huduma ya Maji Duniani World Water-Tech Innovation Summit (WWIS) 2023 London unaoratibiwa na serikali ya Uingereza. Akizungumza katika mkutano Waziri Aweso ametoa wito kwa wadau wa sekta

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga pamoja na ujumbe wa Wizara ya Maji wameshiriki Mkutano maalum unaohusiana na Maswala ya Huduma ya Maji Duniani World Water-Tech Innovation Summit (WWIS) 2023 London unaoratibiwa na serikali ya Uingereza.


Akizungumza katika mkutano Waziri Aweso ametoa wito kwa wadau wa sekta ya Maji duniani kuongeza jitihada katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani ndio changamoto inayokabili dunia kwa sasa. 


Aidha, Katibu Mkuu Eng Sanga akishiriki mjadala wa wataalamu alisisitiza juu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji pamoja na kuwekeza katika uvunaji wa maji ya mvua kwa kujenga mabwawa ili kuhakikisha yanakua sehemu ya kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi. 


Mkutano huu pia, ulijadili namna bora ya kuboresha mifumo ya usambazaji Majisafi na usafi wa mazingira ili kuendana na ongezeko la watu katika maeneo ya mijini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »