WAZIRI MKUU: WATANZANIA TUJIVUNIE UVUMBUZI WA MBEGU MPYA YA MICHIKICHI

WAZIRI MKUU: WATANZANIA TUJIVUNIE UVUMBUZI WA MBEGU MPYA YA MICHIKICHI

Na Mwandishi Wetu kigoma RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUH HASSAN  imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kufanya mageuzi makubwa katika mazao ya mafuta ikiwemo michikichi.Mageuzi haya yanakwenda sambamba na kupanda miche mipya iliyoboreshwa ambayo ina uzalishaji mkubwa wa mafuta. Wana-Kigoma tuamue sasa hivi tupande michikichi

Na Mwandishi Wetu kigoma


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUH HASSAN  imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kufanya mageuzi makubwa katika mazao ya mafuta ikiwemo michikichi.
Mageuzi haya yanakwenda sambamba na kupanda miche mipya iliyoboreshwa ambayo ina uzalishaji mkubwa wa mafuta. Wana-Kigoma tuamue sasa hivi tupande michikichi kwa bidii.


Serikali ilichukua hatua za makusudi za kuliingiza zao la michikichi katika orodha ya mazao ya kimkakati. Mazao mengine ya kimkakati ni pamba, tumbaku, kahawa, korosho, chai, mkonge, zabibu na alizeti.


Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wadau hao, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amesema hayo inaendelea na uzalishaji wa mbegu na miche bora ya michikichi aina ya TENERA inayotoa mafuta mara tatu zaidi ya aina ya DURA ambayo inalimwa na wakulima kwa takribani asilimia 90.
“Hadi kufikia Januari, 2023 TARI Kwa kushirikiana na kampuni binafsi imezalisha jumla ya mbegu milioni 14.14. Kati ya hizi, mbegu milioni 11.59 zimezalishwa na TARI na mbegu milioni 2.54 zimezalishwa na kampuni binafsi zikiwemo FELISA, NDF na Yangu Macho Group Ltd.”


Amesema kati ya mbegu milioni 14.14 zilizozalishwa, mbegu milioni 9.60 zimekwisha sambazwa na kuoteshwa na taasisi mbalimbali zikiwemo JKT na Magereza, Halmashauri zote nane za mkoa wa Kigoma, Halmashauri 25 za nje ya mkoa wa Kigoma, vituo vya TARI na Wakala wa Mbegu za kilimo Tanzania (ASA).
Amesema hadi kufikia Januari, 2023 jumla ya miche 3,122,566 imepatikana ambapo miche 1,968,087 imegawiwa kwa wakulima ndani na nje ya mkoa wa Kigoma.
Mkutano huo wa siku moja bado unaendelea ambapo wakulima na wadau wengine wanaendelea kutoa maoni yao

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »