Wananchi wa Jiji la Dodoma wamshukuru Mbunge wao Mavunde kuwaletea Huduma ya Matibabu ya Macho bure

Wananchi wa Jiji la Dodoma wamshukuru Mbunge wao  Mavunde kuwaletea Huduma ya Matibabu ya Macho bure

Na Barnabas Kisengi  Dodoma Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini  Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Lions Mzizima na  Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwapatia huduma bure ya matibabu ya macho. Wananchi hao wengi wao wakiwa ni wazee wameshukuru kwa huduma hii kwa kuwa wengi wao

Na Barnabas Kisengi  Dodoma


Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini  Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Lions Mzizima na  Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwapatia huduma bure ya matibabu ya macho.


Wananchi hao wengi wao wakiwa ni wazee wameshukuru kwa huduma hii kwa kuwa wengi wao walikuwa wamekata tamaa ya matibabu kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu ya macho.
Mtoto Chrispin Christopher mkazi wa mttaa wa Chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma ambaye alisimama kuendelea na masomo yake baada ya kupata changamoto ya macho iliyompelekea uoni hafifu,amebubujikwa na machozi ya furaha pale ambapo kampeni hii imemrudishia hali yake ya kuona vizuri kama alivyokuwa awali na kuahidi kurejea tena katika masomo yake ili kutimiza malengo yake.

Akizungumza kwaniaba ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Jamal Yared Ngalya amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kupata huduma ya Afya na kuahidi kuendelea kuboresha huduma hii kwa kuleta kambi hizi mara kwa mara ili wananchi wengi zaidi waweze kufikiwa.
“Tutahakikisha Sasa sisi kama Halimashauri ya Jiji la Dodoma tunaendelea kushirikiana na Mh Mbunge kuhakikisha tunakuwa na kambi hizi mara kwa mara katika kata zetu Zote ili tuwarahisishie kupata kwa urahisi huduma za macho na huduma nyingine hii itawasaidia hata wale wasio na uwezo wa kuzimua huduma hizi huku Sasa zitawafikia kwenye kata zenu”Alisisitiza Naibu meya

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »